NA HAMZA TEMBA - WMU.
Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii imeunga mkono uamuzi uliofikiwa na kamati maalum iliyoundwa na Serikali ya Wilaya ya Bagamoyo kwa ajili ya kutafuta suluhu ya kumaliza mgogoro wa ardhi baina ya Hifadhi ya Taifa ya Saadan na wananchi wa kitongoji cha Uvinje walioanzisha makazi ya kudumu ndani ya hifadhi ya Taifa ya Saadan kinyume cha sheria.
Kamati hiyo iliyoundwa na wajumbe watatu ambao ni Serikali ya Wilaya ya Bagamoyo, Uongozi wa Kitongoji cha Uvinje na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania(TANAPA) kupitia Hifadhi ya Taifa ya Saadan ilifikia maazimio kuwa wananchi wa kitongoji hicho walioanzisha makazi ndani hifadhi hiyo waondolewe kwa utaratibu wa kulipwa fidia ili kumaliza mgogoro huo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Wilayani Bagamoyo, Mwenyekii wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii, Mhandisi Atashasta Ndetiye alisema baada ya kutembelea eneo hilo wamejiridhisha kuwa Kitongoji hicho cha Uvinje kimeanzishwa ndani ya eneo la hifadhi ambapo ni kinyume cha sheria. 

"Kiuhalisia tumeona kuna kitongoji ndani ya hifadhi ya Taifa ya Saadan, tumewasikiliza wananchi, tumesikiliza upande wa Serikali, kwa mujibu wa taratibu na sheria wale wananchi wanapaswa watoe ushirikiano, tunaamini kuna taratibu za Kiserikali zinafanywa kuhakikisha wale wananchi wanalipwa ili waondoke kwa usalama" alisema Ndetiye.

Aliongeza, "tumeona jinsi ambavyo baadhi ya wananchi hawako tayari kulipwa, lakini nadhani wakieleweshwa vizuri wataelewa kuwa ile ni hifadhi ya Taifa, na kama ni hifadhi ya Taifa basi inahusu maslahi ya Taifa, hivyo kila mwananchi anatakiwa atoe ushirikiano ili angalao Serikali ifanye uwekezaji wa kueleweka"

Ndetiye alisema kamati hiyo imeshaweka maazimio kwa ajili ya kushauri Bunge ili liazimie ni nini kifanywe na Serikali kumaliza mgogoro huo. Alisema, "Kwa udharura wake na kutokana na maelezo ya mkuu wa Wilaya, kwa ujumla kamati inakubaliana nayo kwasababu ameeleza vitu ambavyo tumeona vina tija zaidi kwa watanzania na tunaenda kulishauri Bunge na Serikali haraka iwezekanavyo ili hatua ziweze kuchukuliwa kumaliza mgogoro huo".
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Aloyce Nzuki (kushoto) akimkaribisha Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mhandisi Atashasta Ndetiye kwa ajili ya kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Saadan hususan eneo lenye mgogoro wa ardhi baina ya kitongoji cha Uvinje na Hifadhi hiyo wakati wa ziara ya kamati hiyo wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani jana. Wananchi wa kitongoji hicho ambao wameweka makazi ndani ya hifadhi hiyo kinyume cha sheria wametakiwa kuondoka kwa hiari katika kipindi cha mwezi mmoja kupisha eneo la hifadhi kabda ya kuondolewa kwa nguvu ambapo watalipwa fidia.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mhandisi Atashasta Ndetiye (wa tatu kushoto) akizungumza na wananchi wa Kitongoji cha Uvinje wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani kuhusu mgogoro wa ardhi baina ya kitongoji hicho na Hifadhi ya Taifa ya Saadan wakati wa ziara ya kamati hiyo wilayani humo jana. Wananchi wa kitongoji hicho ambao wameweka makazi ndani ya hifadhi hiyo kinyume cha sheria wametakiwa kuondoka kwa hiari katika kipindi cha mwezi mmoja kupisha eneo la hifadhi kabda ya kuondolewa kwa nguvu ambapo watalipwa fidia.Wengine pichani ni Naibu Waziri,Wizara ya Maliasili, Mhandisi Ramo Makani(wa pili kulia) na  Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Majid Hemed Mwanga (kulia).
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani (wa tatu kushoto) akiongoza Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kutembelea eneo lenye mgogoro baina ya Kitongoji cha Uvinje na Hifadhi ya Taifa ya Saadan wakati wa ziara ya kamati hiyo kwenye eneo hilo wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani jana. Wananchi wa kitongoji hicho ambao wameweka makazi ndani ya hifadhi hiyo kinyume cha sheria wametakiwa kuondoka kwa hiari katika kipindi cha mwezi mmoja kupisha eneo la hifadhi kabda ya kuondolewa kwa nguvu ambapo watalipwa fidia. Wengine pichani ni Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhandisi Atashasta Ndetiye (wa nne kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Alhaj Majid Hemed Mwanga (wa pili kushoto).
 Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Moses Nnauye (kushoto) akizungumza na wananchi wa Kitongoji cha Uvinje wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani kuhusu mgogoro wa ardhi baina ya kitongoji hicho na Hifadhi ya Taifa ya Saadan wakati wa ziara ya kamati hiyo wilayani humo jana. Wananchi wa kitongoji hicho ambao wameweka makazi ndani ya hifadhi hiyo kinyume cha sheria wametakiwa kuondoka kwa hiari katika kipindi cha mwezi mmoja kupisha eneo la hifadhi kabda ya kuondolewa kwa nguvu ambapo watalipwa fidia.  Wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhandisi Atashasta Ndetiye.





Nyumba inayodaiwa kuwa ni ya muwekezaji anaeshikilia moja ya eneo katika hifadhi ya taifa ya Saadan kwa madai kuwa alipimiwa eneo hilo na Serikali. Taarifa zilitolewa ni kuwa eneo hilo lilipimwa kiholela bila ya kufuata taratibu za kisheria. Hata hivyo licha ya muwekezaji huyo kutoka nchini Botswana kukaa katika eneo hilo kwa zaidi ya miaka tisa ameonekana hajaendeleza eneo hilo kwa lengo lililokusidiwa.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...