Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel ameunga mkono jitihada za ujenzi wa Zahanati na Shule kata za Ludete na Kakubilo Halmashauri ya Geita kwa kuchangia matofali yenye thamani ya shilingi 2,400,000/= na kufanikisha harambee ya mifuko ya Saruji zaidi ya 420.

Mhandisi Robert Gabriel ameunga mkono jitihada za wananchi  baada ya kutembelea kata hizo na kuridhishwa na kazi za ujenzi wa Zahanati za vijiji na Shule zinazofanywa na wananchi kwa kujitolea kufanya kazi bila malipo, kuchangia vifaa mbalimbali vya ujenzi na kuchimba misingi.

Akiwa Kata ya Ludete Mkuu wa Mkoa amesema " Nimefurahi sana kuona namna mnavyoshiriki katika utekelezaji wa miradi hii niwaombe mshiriki kuanzia mwanzo hadi mwisho na msikubali mtu yeyote kuwavunja moyo kwa kuwa maendeleo ya Ludete yataletwa na wananchi wenyewe hivyo mimi ninawachangia matofali 1000 kwa ajili ya Zahanati na mengine 1000 ya kujenga vyumba vya madarasa shule ya Sekondari Ludete".

Mheshimiwa Herman Kapufi Mkuu wa Wilaya ya Geita akitoa maelekezo kwa viongozi wa Halmashauri ya Geita na kata ya kakubilo wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel katika Halmashauri hiyo kuhamasisha ujenzi wa Zahanati na vyumba vya madarasa.
 Mhandisi Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa wa Geita akishirikiana na wananchi wa Kata ya Ludete Wilayani Geita kumwaga zege kwa ajili ya lenta kwenye ujenzi wa madarasa 10 ya shule ya msingi Ludete yenye wanafunzi 6,616  alipokwenda kuzindua kampeni ya ujenzi wa vyumba vya madarasa.

 Mhandisi Robert Gabriel akishirikiana na mafundi kupandisha ndoo yenye zege kwa ajili ya uwagaji wa leta katika majengo 10 ya vyumba vya madarasa shule ya Msingi Ludete Wilayani Geita.

 Mhandisi Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa Geita akikabidhi fedha shilingi 2,400,000/= kwa Diwani wa Kata ya Ludete Sebastian Mranda kwa ajili ya ujenzi wa boma la Zahanati ya Kijiji na Ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari katika hiyo.
 Wananchi wa kijiji cha Ludete Kata ya Ludete Wilayani Geita wakishiriki katika uchimbaji wa msingi kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati katika kijiji hicho kwa lengo la kuunga mkono jitihada za mkuu wa mkoa wa Geita za kila kijiji kuwa na Zahanati.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...