Baada ya malalamiko ya muda mrefu, hatimae mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) amerejesha TAKUKURU Jalada la uchunguzi la kesi ya utakatishaji wa USD 300,000, inayowakabili Rais wa klabu ya Simba, Evans Aveva na Makamu wake,Godfrey Nyange maarufu kama Kaburu na kuelekeza uchunguzi zaidi ufanyike.

Mwendesha Mashtaka Mwandamizi wa Takukuru, Leonard Swai ameewleza hayo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Victoria Nongwa kesi hiyo ilipokuja kutajwa,

Pia alidai kuwa jalada la kesi hiyo lililokuwepo kwa DPP limekwisha rejeshwa na ameelekeza uchunguzi zaidi ufanyike  na kwamba uchunguzi huo umekwishaanza kuwa ajili ya kukamilisha maeneo ambayo DPP ameelekeza.

Aidha amedai wanaomba ufunguo kutoka kwa mshtakiwa Aveva ili waweze kupata nyaraka ikiwa sehemu ya kukamilisha upelelezi.

Amedai Aveva alikuwa na ofisi mbili, ya Simba na binafsi na kwamba katika ofisi  hiyo binafsi kuna nyaraka za Simba na kuwa walimuandikia barua kupitia gerezani ili aweze kuruhusu upatikanaji wa funguo ili wapate nyaraka zinazohitajika lakini hawajajibiwa.  Swai aliomba upande wa utetezi uharakishe wapate hizo nyaraka ili waweze kukamilisha upelelezi.

Wakili wa utetezi, Evodius Mtawala aliieleza mahakama kuwa  Aveva ameipata barua hiyo na kwamba juhudi zinaendelea kufanyika na nyaraka zilizoombwa zinaendelea kukusanywa na zitawasilishwa hivi karibuni.

Baada ya kutolewa maelezo hayo, Hakimu Nongwa ameahirisha kesi hadi Desemba 28, mwaka huu.

Katika kesi hiyo, Evans Aveva na makamu wake, Kaburu wanakabiliwa na mashtaka matano ya kughushi, kuwasilisha nyaraka ya uongo na kutakatisha fedha USD 300,000.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...