Mfuko
wa Pensheni wa LAPF umepata tuzo ya uandaaji bora wa hesabu katika
sekta ya Hifadhi ya Jamii na Bima kwa mwaka 2015/16 inayotolewa na Bodi
ya Taifa ya Uhasibu (NBAA).
Akizungumza
na waandishi wa habari leo Mjini Dodoma kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu
wa Mfuko huo Bw. Eliud Sanga, Mkurugenzi wa fedha wa Mfuko huo Bw. John
Kida amesema kuwa mfuko huo umepata tuzo hiyo kwa miaka saba mfululizo
ikiwa ni ishara ya utendaji mzuri na wenye kuchochea ukuaji wa Mfuko na
maendeleo ya Taifa kwa ujumla kutokana na uwekezaji unaofanywa katika
sekta mbalimbali.
“Kwa
mwaka 2015/2016 mapato yanayotokana na uwekezaji katika vitega uchumi
yalifikia shilingi bilioni 96.03 ikilinganishwa na shilingi bilioni
72.72 kwa mwaka 2014/2015 ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 32.”
Alisisitiza Kida .Akifafanua
Kida amesema kuwa mafanikio ya mfuko huo yanatokana na kuongezeka kwa
wanachama ambao hadi Septemba 2017 walikuwa wamefikia 180,401.
Aliongeza
kuwa Mfuko huo katika kipindi cha mwaka 2015/2016 umelipa mafao kwa
wanachama 8,011 ambapo jumla ya shilingi bilioni 107.24 zililipwa kama
mafao kwa wanachama.
Akieleza
mafanikio mengine Kida amesema kuwa michango ya wanachama imeongezeka
ambapo kwa mwaka 2015/2016 imefikia shilingi bilioni 279.68
ikilinganishwa na shilingi bilioni 210.07 sawa na ongezeko la asilimia
33 hali iliyosababishwa na kuoongezeka kwa wanachama kutoka 150,835 hadi
kufikia wanachama 166,260 mwezi June 2016.
Kwa
upande wake Meneja Masoko na Uhusiano wa Mfuko huo Bw. James Mlowe
amesema mafanikio ya mfuko huo yanatokana na utendaji makini
unaozingatia utawala Bora katika kusimamia rasilimali za Mfuko huo
ikiwemo fedha. Mfuko wa Pensheni wa LAPF umewekeza katika vitega uchumi
mbalimbali ambapo hadi kufikia June 2016 ulikuwa umewekeza jumla ya
shilingi trilioni 1.09, wakati kwa kipindi cha mwezi June 2015 mfuko huo
uliwekeza bilioni 884.26 katika vitega uchumi mbalimbali kama dhamana
za Serikali, Amana za mabenki, majengo, hisa za makampuni na uwekezaji
katika Kampuni tanzu.
Mkurugenzi wa Fedha wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF Bw. John Kida akizungumza na waandishi kuhusu mfuko huo kupata tuzo ya uandaaji bora wa hesabu katika sekta ya hifadhi ya Jamii na Bima ya Afya kwa mwaka 2015/2016 ambapo Mfuko huo umeshika nafasi ya kwanza, Tuzo hiyo imetolewa na Bodi ya Taifa ya Uhasibu (NBAA) hivi karibuni.Kulia ni Meneja Masoko na Uhusiano wa LAPF Bw. James Mlowe.
Meneja Masoko na Uhusiano wa LAPF Bw. James Mlowe akieleza mikakati iliyouwezesha mfuko huo kupata tuzo hiyo ikiwemo uwajibikaji na utawala bora katika kusimamia rasilimali fedha katika mfuko huo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Fedha wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF Bw. John Kida.
Mkurugenzi wa Fedha wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF Bw. John Kida (Katikati) akionesha kwa waandishi wa habari ( hawapo pichani) tuzo ya uandaaji bora wa hesabu katika sekta ya hifadhi ya Jamii na Bima ya Afya kwa mwaka 2015/2016 ambapo Mfuko huo umeshika nafasi ya kwanza, Tuzo hiyo imetolewa na Bodi ya Taifa ya Uhasibu (NBAA) hivi karibuni.
Meneja Masoko na Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF Bw. James Mlowe akifurahia tuzo ya uandaaji bora wa hesabu katika sekta ya hifadhi ya Jamii na Bima ya Afya kwa mwaka 2015/2016 ambapo Mfuko huo umeshika nafasi ya kwanza, Tuzo hiyo inatolewa na Bodi ya Taifa ya Uhasibu (NBAA) hivi karibuni.
Meneja Matekelezo wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF Bw. Victor Kikoti (Wakwanza) akieleza kwa waandishi wa habari (hawapo pichani ) kuhusu mafao yanayotolewa na mfuko huo na faida wanazopata wananchi kutokana na mafao hayo .(Picha zote na LAPF).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...