Katibu MKuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza mapema jana kwenye mkutano wa Halmashauri kuu ya Wilaya uliokuwa ukifanyika jana katika kata ya Ilongero,Singida vijijini katika jimbo la Singida Kaskazini,ambapo Wajumbe wa CCM walikuwa wakipiga kura kutafuta Mbunge atakaekiwakilisha chama hicho katika uchaguzi Mdogo wa Ubunge unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni,kufuatia jimbo hilo kuachwa wazi na aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo Mh.Lazaro Nyalandu aliyehamia CHADEMA.Ndugu Kinana aliwaasa Wajumbe hao kumchagua mtu anaefaa na atakawasaidia na kuwasemea matatizo yao,na atakae kuwa tayari kuwaletea maendeleo.

Kina pia aliwaasa Wana CCM kumuunga mkono Mwenyekiti wao,Rais Dkt John Pombe Magufuli katika suala zima la kupambana na vita ya rushwa,ufisadi,ubadhirifu wa mali za umma na kuhakikisha nidhamu ndani ya chama na watumishi wa umma inaimarika kwa kiwango kikubwa.
Wajumbe wakimsikiliza Ndugu Kinana kwa umakini kwenye mkutano huo.
Baadhi ya Wananchi waliovutiwa na hotuba ya Katibu Mkuu Ndugu Kinana,ilibidi wasogee zaidi na kuendelea kusikiliza
Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Singida Ndugu Juma Kilimba akimkaribisha Mgeni rasmi,Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana aliyepita kuwasalimia na kuona wamejiandaaje na uchaguzi wao wa kura za maoni kwa ajili ya kumchagu Mtu atakaewawakilisha katika uchaguzi Mdogo wa Ubunge unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni,kufuatia jimbo hilo kuachwa wazi na aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo Mh.Lazaro Nyalandu aliyehamia CHADEMA.Ndugu Kinana aliwaasa Wajumbe hao kumchagua mtua anaefaa na atakawasaidia na kuwasemea matatizo yao,na atakae kuwa tayari kuwaletea maendeleo.
 Wajumbe wa Halmashauri kuu ya Wilaya ya Singida Vijijini wakishangilia jambo,wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahamani Kinana alipokuwa akizungumza nao kabla ya kupiga kura ya kumchagua atakaewawakilisha katika nafasi ya Ubunge,na hatimaye kugombea katika uchaguzi mdogo wa Ubunge unaotarajiwa kufanyika jimboni humo hivi karibuni.
Mjumbe wa kamati kuu ya siasa ya Mkoa,Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dkt Rehema Nchimbi akizungumza mapema jana kwenye mkutano wa Halmashauri kuu ya Wilaya uliokuwa ukifanyika jana katika kata ya Ilongero,Singida vijijini katika jimbo la Singida la Kaskazini,ambapo Chama cha Mapinduzi kinamtafuta Mbunge atakaekiwakilisha chama hicho katika uchaguzi Mdogo wa Ubunge unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni,kufuatia jimbo hilo kuachwa wazi na aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo Mh.Lazaro Nyalandu aliyehamia CHADEMA. 


 Katibu MKuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mjumbe wa kamati kuu ya siasa ya Mkoa,Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dkt Rehema Nchimbi jana mara baada ya kuwasili katika Kata ya Ilongero,Singida vijijini katika jimbo la Singida la Kaskazini,ambapo Chama cha Mapinduzi jana kilikuwa kinapiga kura za maoni kumchagu Mbunge atakaekiwakilisha chama hicho katika uchaguzi Mdogo wa Ubunge unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni,kufuatia jimbo hilo kuachwa wazi na aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo Mh.Lazaro Nyalandu aliyehamia CHADEMA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...