KAIMU Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya, Dkt. Yahya Msuya, (pichani juu), amewataka madaktari na watoa huduma za afya, waliokuwa wakishiriki mafunzo ya wiki moja ya kufanya tathmini ya ulemavu kwa wafanyakazi watakaoumia au kuugua kutokana na kazi zao, kutumia elimu waliyoipata kwa ufanisi na weledi.

Akifunga mafunzo hayo ya siku tano yaliyoratiubiwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), ili kuwajengea uwezo wataalamu hao wa afya, Dkt. Msuya alisema, ni ukweli kwamba Mfuko wa WCF hauna muda mrefu tangu uanzishwe na serikali na kwa mantiki hiyo, mkakati wa mafunzo ni muhimu ili kuhakikisha kwamba wadau wote wanaonufaika au kuwajibika na Mfuko kuelewa shughuli zake na kuhakikisha kwamba lengo la kuanzishwa kwa Mfuko huo linatimia.

“Nahakika katika kipindi hiki mlichokuwepo hapa mtakuwa mmejifunza mambo mengi mapya na kuwapa ujuzi ambao huenda hamkuwa nao wakati mnakuja hapa.” Alsiema Dkt. Msuya.

Kwaupande wake, Mratibu wa mafunzo hayo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Tiba na
Tathmini wa WCF, Dkt. Abdulsalaam Omar, alisema, lengo kuu ni kuwaelimisha
madaktari kufanya tathmini ya ulemavu kwa wafanyakazi watakaoumia au kuugua
kutokana na kazi zao kwenye maeneo yao ya kazi ili kutoa mapendekezo kwa Mfuko
kwa ajili ya uamuzi wa mwisho wa kutoa fidia. “Washiriki 85 kutoka mikoa ya
kanda ya nyanda za juu kusini wameshiriki na tuna hakika pamoja na elimu waliyoipata lakini pia watakuwa mabalozi wetu wazuri watakaporejea kwenye maeneo yao ya kazi.” Alisema Dkt. Omar.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano WCF, Bi. Laura Kunenge, amesema, kila mshiriki amepatiwa cheti cha ushiriki na stika atakayokwenda kuibandika kwenye ofisi
yake kwa nia ya utambuzi wa mtoa huduma ya tathmini.“Stika hizi zinamuelekea mteja kuwa ofisi hiyo anapatikana daktari aliyepatiwa mafunzo ya kufanya tathmini ya mfanyakazi aliyeumia au kupata maradhi mahala pa kazi.”Alifafanua Bi. Laura.
Madaktari na watoa huduma za afya kutoka mikoa ya nyanda za juu Kusini, waliokuwa wakishiriki mafunzo ya wiki moja ya kufanya tathmini kwa mfanyakazi aliyeumia mahala pa kazi, wakionyesha stika watakazobandika maofisini kwao, zikionyesha ofisi ya mtoa huduma, mwishoni mwa mafunzo hayo yaliyoratibiwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, WCF na kufanyika jijini Mbeya Desemba 15, 2017. 


NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

Mgeni rasmi Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya, Dkt. Yahya Msuya, (wapili kulia), akimkabidhi cheti cha ushiriki Dkt. Rehema Mwanga. wanaoshuhudia ni Mratibu wa mafunzo, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Tiba na Tathmini wa WCF, Dkt. Abdulsalaam Omar, (kulia), na kiongozi wa timu ya wawezeshaji, Daktarin bingwa na mbobezi wa mifupa na viungo, Dkt. Robert Mhina.
Washiriki wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasilianoi WCF, Bi. Laura Kunenge, (kulia), akimkabidhi cheti mmoja wa washiriki, Dkt. Gloria Mbwile, ambaye ni mganga mfawidhi hospitali ya mkoa wa Mbeya.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...