WATOTO wanaolelelewa katika vituo vya kulea watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira hatarishi wametakiwa kujitambua na kujikubali ili kutekeleza wajibu wao wa kupokea malezi mema. Aidha imeelezwa kuwa watoto wanathaminika sana ndio maana wapo watu wameamua kujitolea kuhakikisha wanaishi maisha ya kawaida na kuwa watu muhimu katika jamii. Kauli hiyo imetolewa na Mchungaji msaidizi, Faith Tetemeko wa Kanisa la Ukombozi tawi la Dar es Salaam, wakati akizungumza na watoto wa wa kituo cha Watoto Wetu Tanzania kilichopo Mbezi Luis hivi karibuni. akimkabidhi Mama mlezi wa kituo cha yatima cha Watoto Wetu Tanzania kilichopo Mbezi Luis, wilaya ya Ubungo mkoani Dar es salaam, Getrude Nyalubamba (kushoto) akiwa ameongozana na Mwenyekiti kamati ya Msamaria mwema ya kanisa la Ukombozi, Leonard Masano (kulia) walipowasili kituoni hapo kwa ajili ya kukabidhi misaada mbalimbali.[/caption] Mchungaji huyo na kundi la wanawake na wanaume wa kanisa hilo walifika kituoni hapo kutembelea watoto hao na kuwapa zawadi mbalimbali. Alisema katika hafla hiyo kwamba watoto hao wanapojiamini, kujikubali na kujithamini wataona manufaa yake hasa kwa kukubali malezi na kutambua uwepo wa walezi ambao wanajali maslahi yao. Aidha alisema kwamba ni wajibu wa jamii na kanisa kwa ujumla kutekeleza kwa vitendo kujali yatima wajane na wale wanaoishi katika mazingira hatarishi kwa kuwa kitendo hicho kina Baraka kubwa. Mchungaji msaidizi, Faith Tetemeko (kulia) wa Kanisa la Ukombozi, akibeba gunia la unga kuingiza katika eneo la kituo cha yatima cha Watoto Wetu Tanzania kilichopo Mbezi Luis, wilaya ya Ubungo mkoani Dar es salaam hivi karibuni. Anayemsaidia ni mmoja wa wakazi wa kituo hicho Elizabeth Samweli anayesoma shule ya sekondari ya Pomerini, Iringa. Wanawake na wababa wa kanisa la Ukombozi walifika kituoni hapo wakiongozwa na mchungaji huyo kwa ajili ya kutoa misaada mbalimbali.[/caption] Alisema kwamba amefurahishwa kufika katika kituo hicho na kutekeleza wajibu wa kukaa pamoja na watoto hao na kumpongeza mama mlezi kwa kazi yake kubwa anayoifanya katika kuwahudumia watoto takribani 31 wanaoishi hapo. Aliwataka watanzania kuwa na tabia ya kujali watoto hao kwa kuhakikisha wanapata mahitaji yao kila siku na sio siku ya sikukuu tu. Kituo cha Watoto Wetu Tanzania kilihamishwa kutoka Stop Over kwenda Mbezi Luishi ili kupisha matakwa ya sheria ya barabara ya Morogoro. 

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...