Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(kushoto) akikabidhi vitabu vya matayarisho ya awali ya kuwaandaa wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa elimu ya sekondari (baseline course), kwa Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya Mji Bariadi, Mwl. Esthom Makyara vilivyotolewa na wadau wa Elimu, wakati wa zoezi la ugawaji wa vitabu hivyo lililofanyika kimkoa Mjini Bariadi.
Na Stella Kalinga, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu
Wizara ya Elimu pamoja na wadau wengine wa Elimu wametoa vitabu 16,985 kwa
shule za Sekondari za Mkoa wa Simiyu kwa ajili ya matayarisho ya awali ya
kuwaandaa wanafunzi wa kidato cha kwanza na elimu ya sekondari (baseline
course).
Akikabidhi vitabu hivyo kwa Maafisa Elimu wa Halmashauri zote sita za Mkoa wa Simiyu,
Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka amesema vitabu hivyo ni msaada mkubwa kwa
Mkoa huo, vikitumiwa vizuri na walimu wenye nia ya kufanya mapinduzi ya elimu na
kuwasaidia wanafunzi kujua maana halisi ya vitabu hivyo, vitasaidia Mkoa wa Simiyu
kufikia malengo ya kiushindani katika Elimu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na Maafisa Elimu Sekondari na baaadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Bariadi(hawapo pichani), kabla ya kukabidhi vitabu vya matayarisho ya awali ya kuwaandaa wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa elimu ya sekondari (baseline course), kwa maafisa elimu wilaya vilivyotolewa na wadau mbaimbali wa Elimu.
Ameongeza kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa wanafunzi wanapata vitabu
pamoja na mahitaji mengine ikiwa ni pamoja na madawati, walimu, vyumba vya
madarasa vinavyotolesheleza hivyo akasisitiza vitabu hivyo vikatumike kwa kusoma
ili viwasaidie.
“Vitabu hivi mtakapogawiwa mkavitumie kwa ajili ya kusoma visiwe mapambo na
kama mwanafunzi hujui uliza, jibidiishe kujua kitabu hicho kinahusu nini na kama
hujaelewa muulize mwalimu ili kesho kwenye mtihani ufaulu kama wenzako
wananvyofaulu” alisema Mtaka.
Aidha, Mtaka amewataka Maafisa Elimu mkoani humo kuzungumza na walimu kabla
ya kugawa vitabu hivyo ili vitakapogawiwa katika shule vigawiwe katika utaratibu
mzuri utakowawezesha walimu kuwasadia wanafunzi kuvitumia kwa manufaa.
Akitoa taarifa juu mapokezi ya vikao hivyo Katibu Tawala Mkoa amesema Mkoa huo
umepokea jumla ya vitabu 16,000 kwa ajili ya wanafunzi na vitabu 985 kwa ajili
walimu(kiongozi cha mwalimu).
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(kushoto) akikabidhi vitabu vya matayarisho ya awali ya kuwaandaa wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa elimu ya sekondari (baseline course), kwa Afisa Elimu (Sekondari) wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Mwl. Jumanne Yasini vilivyotolewa na wadau wa Elimu, wakati wa zoezi la ugawaji wa vitabu hivyo lililofanyika kimkoa Mjini Bariadi.
Akizungumza kwa niaba ya Maafisa Elimu Sekondari mkoani humo, Afisa Elimu
Sekondari wa Halmahauri ya Mji Bariadi Mwl. Esthom Makyara amesema vitabu
hivyo ni msingi mzuri kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza na Maafisa Elimu hao
wanapaswa kuwaelekezaWakuu wa shule kutofungia vitabu hivyo stoo badala yake
wanafunzi wapewe ili wavisome.
Naye Kaimu Afisa Elimu Mkoa wa Simiyu, Ndg.Charles Maganga amesema Maafisa
Elimu Sekondari wahakikishe vitabu hivyo vinagawiwa kwa wakuu wa shule kabla ya
shule kufunguliwa Januari 08, 2018, ili wanafunzi wa kidato cha kwanza wanapoanza
masomo wavikute shuleni.
Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Bariadi
walioshuhudia zoezi la ugawaji wa vitabu hivyo kimkoa wamesema, vitabu hivyo
vitawasaidia wenzao wa kidato cha kwanza kujenga msingi mzuri wa maarifa ya
jumla na lugha ya Kiingereza.
Vitabu hivi vimetolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na
Msaada wa Watu wa Marekani(UKAID) kupitia Mpango wa Taifa wa Kuinua Ubora
wa Elimu hapa nchini EQUIP-T.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(kushoto) akikabidhi vitabu vya matayarisho ya
awali ya kuwaandaa wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa elimu ya sekondari (baseline course), kwa Afisa
Elimu (Sekondari) wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, Mwl. Joseph Mashauri vilivyotolewa na wadau wa
Elimu, wakati wa zoezi la ugawaji wa vitabu hivyo lililofanyika kimkoa Mjini Bariadi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...