Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

JALADA la kesi inayomkabili Mhasibu Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU), Godfrey Gugai anayedaiwa kumiliki mali zenye thamani ya Sh.bilioni 3 ambazo haziendani na kipato chake, bado lipo mikononi kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwa ajili ya kulipitia na kulitolea maamuzi.

Wakili wa Serikali, Vitalis Peter amedai hayo leo mbele ya Hakimu Mkazi mkuu, Thomas Simba wakati shauri hilo lilipokuja kwa ajili ya kutajwa.Awali, jalada hilo lilipelekwa kwa DPP ambapo alilipitia na kulirejesha TAKUKURU na kuelekeza baadhi ya maeneo yafanyiwe uchunguzi zaidi na kisha kurudishwa kwa DPP.

Alidai maeneo hayo yamekwishafanyiwa kazi na jalada limerejeshwa tena kwa DPP kwa ajili ya kulipitia na kulitolea maamuzi.Hata hivyo, Wakili wa Utetezi, Alex Mgongolwa alidai kesi hiyo imekuwa ya muda mrefu na kila siku wanaambiwa upelelezi haujakamilika na jalada lipo kwa DPP.

" Tunaomba tarehe ijayo upande wa mashtaka watueleze wamefikia wapi upelelezi, ili kesi hii iweze kuendelea na hatua nyingine, kwa sababu wateja wangu gerezani.Baada ya kueleza hayo, Hakimu Simba aliutaka upande wa mashtaka kukamilisha upelelezi haraka ili kesi hiyo iendelee na hatua nyingine.

Hakimu Simba alisema " Katika kesi hii sitakuwa na utani , nataka kesi hii itakaporudi, upande wa mashtaka mje na maelezo ya kujitosheleza" alisema na kuongeza kuwa " Sitaki kesi hii ichukue muda mrefu, nataka upande wa mashtaka mhakikishe upelelezi unakamilika kwa haraka, maana upelelezi usipokamilika haraka, jamii inachukulia kuwa mahakama ndio inachelewesha kesi," amesema.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 6, mwaka 2018, Mbali na Gugai, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni George Makaranga, Leonard Aloys na Yasini Katera. Washtakiwa hao wanaokabiliwa na mashtaka 43 yakiwemo 20 ya utakatishaji fedha haramu, kumiliki mali zisizoendana na kipato na kughushi mikataba ya mauziano ya viwanja katika maeneo mbalimbali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...