Na Ismail Ngayonga
NAIBU Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa amewataka Watendaji wa Taasisi zilizopo chini ya Wizara hiyo kutumia weledi, maarifa na ujuzi walionao ili kufanikisha adhma ya Tanzania kuwa nchi ya kipato cha kati kupitia uchumi wa viwanda.
Akizungumza katika kikao cha majumuisho ya Zaira yake ya kukagua miradi ya sekta ya ujenzi Mkoani Tanga na Watendaji wa Wizara hiyo, jana Alhamisi Februari 15, 2018, Naibu Waziri Kwandikwa amewataka Watendaji hao kubuni mipango na mikakati mbalimbali itayoweza kulisaidia Taifa.
Alisema Watendaji wa Taasisi zilizopo chini ya Wizara hiyo ikiwemo Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) na Wakala wa Ufundi na Umeme Serikalini (TEMESA) wana wajibu mkubwa wa kutimiza matarajio hayo yaliyowekwa na Serikali katika kufikia nchi ya kipato cha kati.
Kwa mujibu wa Kwandikwa alisema, Wizara hiyo imekuwa na watalaamu wa kutosha na wenye weledi ambao wamekuwa tegemeo kubwa katika Taifa, hivyo ni wajibu wa Watendaji hao kufanya kazi kwa bidii kwa kutumia vipaji vyao badala ya kuacha ujuzi na maarifa waliyonayo yakipotea bila ya kuinufaisha.
“Wizara hii, imekuwa tegemeo katika sekta zote za kiuchumi, hususani wahandisi tulionao katika Taasisi zetu, hivyo ni vyema tuhakikishe kuwa utaalamu huu unaweza kuleta matokeo chanya katika Taifa letu ikizingatia kuwa Tanzania ya Uchumi wa Viwanda itagemea sana Wataalamu wengi kutoka Wizara yetu” alisema Kwandikwa.
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa akisalimiana
na Watendaji wa Taasisi zilizopo chini ya Wizara hiyo ikiwemo TBA,
TANROADS na TEMESA wakati wa mkutano wa majumuisho ya ziara yake ya
kukagua miradi mbalimbali ya sekta za ujenzi inayosimamiwa na Wizara
hiyo jana Alhamisi Februari 15, 2018. Kulia kwake ni Meneja wa TANROAD
Mkoa wa Tanga, Mhandisi Alfred Ndumbaro.
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa akizungumza
na Watendaji wa Taasisi zilizopo chini ya Wizara hiyo ikiwemo TBA,
TANROADS na TEMESA wakati wa mkutano wa majumuisho ya ziara yake ya
kukagua miradi mbalimbali ya sekta za ujenzi inayosimamiwa na Wizara
hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...