Kamati ya Maadili ilikutana tarehe 14/3/2018 kupitia shauri linalomhusu Ndugu Michael Richard Wambura, Makamu Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) ambaye anashtakiwa na Sekretarieti ya TFF kwa makosa matatu ya kimaadili.

TUHUMA ZILIZOWASILISHWA
Sekretarieti ya TFF iliwasilisha mbele ya Kamati mashtaka matatu (3) ambayo ni;

1.    Kupokea/kuchukua fedha za Shirikisho (TFF) za malipo ambayo  hayakuwa halali ikiwa ni kinyume na kifungu cha 73(1) cha Kanuni za Maadili za TFF Toleo la 2013.

2.    Kughushi barua ya kuelekeza alipwe malipo ya kampuni ya JEKC SYSTEMS LIMITED huku akijua malipo hayo sio halali ikiwa ni kinyume na kifungu cha 73(7) cha Kanuni za Maadili za TFF Toleo la 2013.

3.    Kufanya vitendo vinavyoshusha Hadhi ya Shirikisho ikiwa ni kinyume na ibara ya 50(1) ya Katiba ya TFF (kama ilivyorekebishwa 2015)

MAELEZO YA KOSA

Ndugu Michael Richard Wambura alichukua fedha isivyo halali kwa kughushi barua ya kampuni ya JEKC SYSTEMS LIMITED ya kujipa mamlaka ya kulipwa kwa kula njama na waliokuwa Viongozi Wakuu wa TFF; Rais na Katibu Mkuu waliopita. Kitendo hiki ni kuvunja maadili na kushusha hadhi ya Taasisi ya TFF.

SHAURI LILIVYOENDESHWA

Ndugu Wambura alipelekewa wito wa kufika mbele ya Kamati siku ya tarehe 14/3/2018 ili awasilishe utetezi kuhusu tuhuma zinazomkabili. Ndugu Wambura alipewa hiari ya kutoa utetezi huo kwa mdomo, kutuma kwa maandishi, kuleta mashahidi au kutuma mwakilishi kama kifungu cha 58 cha Kanuni za Maadili za TFF toleo la 2013 kinavyoelekeza. Ndugu Wambura alimtuma mwakilishi wake, Wakili Emanuel Muga, aliyefika na kuthibitisha kuwa ametumwa na mteja wake (Ndugu Michael Richard Wambura) kuwasilisha utetezi wake mbele ya Kamati.

Baada ya kuelezwa mashtaka yanayomkabili mteja wake, Wakili Muga aliiomba Kamati kuwa mteja wake anaomba kupewa muda wa kupitia shauri hilo ili aandae utetezi, vielelezo, na mashahidi. Mara baada ya kutoa ombi hilo Kamati ilimruhusu asubiri ili ipitie kabla ya kufanya uamuzi. Baada ya majadiliano wajumbe walikubaliana kuwa suala hili si geni kwa Ndugu Wambura; hivyo siyo kweli kuwa hana ufahamu nalo. 


Pia moja ya vielelezo vilivyowasilishwa mbele ya Kamati ni utetezi wa maandishi wa Ndugu Wambura kuhusiana na suala hilo ulioandikwa 4/12/2017. Hivyo Kamati ilijiridhisha kuwa Ndugu Wambura anao ufahamu wa kutosha wa suala hilo na alikuwa na uwezo wa kufika mbele ya Kamati ili kutoa maelezo ya ziada.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...