BODI ya wadhamini ya Hospitali ya Taifa Muhimbili pamoja na Menejimenti yake imejiwekea mikakati mbalimbali katika mpango mkakati wake wa miaka mitano kuanzia mwaka 2017 hadi mwaka 2022 unaolenga kuimarisha utawala bora ambao ni muhimu katika utekelezaji wa mikakakati mingine inayolenga kuboresha huduma kwa wagonjwa.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Dk. Ellen Mkondya-Senkoro wakati akizindua Kamati mbili ya Kudhibiti Uadilifu na Uratibu.

Amesema pamoja na ueledi wa kazi, uadilifu katika utumishi wa umma ni pamoja na kutokuomba rushwa au kutoa rushwa wakati watumishi wa umma wanapotekeleza majukumu yao. "Hospitali ya Taifa Muhimbili inaunga mkono mkakati wa Taifa dhidi ya rushwa na mpango mkakati wa utekelezaji wa awamu ya tatu (2017-2022).

"Nina imani kwamba kamati hizi zitatekeleza majukumu yake ipasavyo kuhakikisha kwamba mkakati huu unatekelezwa kwa mujibu wa maelekezo ya Serikali," amesema Dk. Mkondya-Senkoro.

akamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini (MNH), Dkt. Ellen Mkondya-Senkoro wakati akizindua Kamati mbili ya Kudhibiti Uadilifu na Uratibu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru (katikati) akitambulisha viongozi na wajumbe wa Kamati mbili ya Kudhibiti Uadilifu na Uratibu.

Viongozi wa kamati ya Kamati mbili ya Kudhibiti Uadilifu na Uratibu wakijitambulisha.
Viongozi wakifuatilia uzinduzi huo.
Kiongozi kutoka idara ya utawala bora, ofisi ya Rais, Ikulu kwa kushirikiana na taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) wakitoa mafunzo elekezi na wawezeshaji kwa kamati zilizochaguliwa.

Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Dk. Ellen Mkondya-Senkoro (wa tatu toka kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi na wajumbe wa kamati mbili zilizochaguliwa. Picha/Habari: Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...