Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma
Serikali ya Kuwait kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Kuwait (Kuwait for Arab Economic Development Fund), imeahidi kuipatia Tanzania mkopo wenye masharti nafuu wa dola milioni 207.3, sawa na shilingi bilioni 466.4, kwa ajili ya ujenzi wa barabara za mzunguko wa kuingia katikati ya mji wa Dodoma pamoja na mradi wa ujenzi wa barabara kutoka Morogoro hadi Dodoma, yenye urefu wa kilometa 257.

Ahadi hiyo imetolewa mjini Dodoma na Balozi wa Kuwait hapa nchini, Mhe. Jassem Ibrahim Al-Najem, alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango.

Balozi Al-Najem amesema kuwa mradi wa ujenzi wa barabara za mzunguko za kuingia na kutoka mjini Dodoma zitasaidia kuondoa msongamano wa magari yanayopita katikati ya mji huo kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu na vyombo vya moto baada ya Makao Makuu ya Serikali kuhamia Dodoma.

Aliahidi kuwa nchi yake kupitia Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait na taasisi washirika (Mifuko ya Waarabu) wa mfuko huo, wataendelea kushirikiana na Tanzania kwa kutoa ufadhili wa ujenzi wa miradi mbalimbali ikiwemo ya miundombinu na kilimo ili iweze kukuza uchumi na maisha ya watu wake.

Katika kipindi cha miaka 40, Serikali ya Kuwait, kupitia Kuwait Fund, imeipatia Tanzania mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 608 kwa ajili ya kutekeleza miradi 14 ya kiuchumi katika sekta za barabara, kilimo, umeme, Maji na Afya.
 Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jassem Al-Najem, akizungumzia uhusiano mzuri ambao umeendelea kuwepo kati ya Tanzania na Kuwait alipomtembelea Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb)(hayupo pichani), ofisini kwake Mjini Dodoma.
 Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Mhe. Jassem Al-Najem (kulia) akimkabidhi zawadi Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) alipomtembelea kwa mazungumzo Mjini Dodoma.
 Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Mhe. Jassem Al-Najem (kulia) akiagana na mwenyeji wake  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) alipomtembelea Mjini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) akizungumza jambo na Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. John Rubuga (katikati) baada ya kuagana na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jassem Al-Najem (hayupo pichani) alipomtembelea Ofisini kwake Mjini Dodoma.

KUSOMA ZAIDI  BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...