Na Ripota Wetu, Globu ya jamii
WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema ni marufuku kwa madaktari kujaza fomu za uchunguzi wa afya bila kupima wanafunzi husika iwapo ana ugonjwa wa Kifua Kikuu(TB) au laa kwani kufanya hivyo ni kuliangamiza kwa makusudi Taifa kwa uzembe ambao hauwezi kuvumilika.

Pia amesema Serikali inatambua umuhimu wa ushirikishwaji wa jamii katika mapambano ya kutokomeza TB na huku akieleza mpaka sasa takribani watoa huduma 1530 kati ya 5000 katika ngazi ya jamii ambao wamepata mafunzo ya muda mfupi ya Kifua Kikuu na hivyo wanaweza kuwabaini wagonjwa wa TB na kuwafuatilia watoto wanaopata matibabu katika maeneo yao.

Waziri Mwalimu ametoa kauli hiyo leo kwenye tamko lake   kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya TB duniani ambayo hufanyika Machi 24 ya kila mwaka ambapo amefafanua TB ni ugonjwa wa kuambukiza ambao unaoongoza kwa kusababisha vifo vingi duniani.

Hivyo amasema ili kukabiliana na ugonjwa huo pamoja na hatua mbalimbali zinazochukuliwa amewaagiza waganga wafawidhi wote wa hospitali na vituo vya huduma kuhakikisha watoto wote wanaoanza shule za bweni wanafanyiwa uchunguzi wa TB kikamilifu kabla ya kuanza masomo.

 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (MB) akisisitiza jambo mbele ya Waandishi wa Habari (Hawapo kwenye Picha), wakati wa Maazimisho ya siku ya Kifua Kikuu Duniani, tukio limefanyika mapema leo katika ukumbi wa Habari Maelezo jijini Dodoma.
Baadhiya  Waandishi wa Habari wakifuatilia kwa ukaribu tamko la Kifua Kikuu (TB) lililokuwa linatolewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (MB) katika ukumbi wa Habari Maelezo jijini Dodoma mapema leo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...