Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema uamuzi wa maombi ya dhamana katika kesi  ya kuhujumu uchumi inayomkabili mfanyakazi mstaafu wa Shirika la Mafuta Tanzania na Zambia(Tazama),  Samwel Nyakirang'ani(63) na wenzake sita, kujulikana Aprili 5, mwaka huu.

Uamuzi huo ambao ulitakiwa kutolewa leo, umeahirishwa kwa sababu Hakimu Mkazi Mkuu,Thomas Simba amesema bado hajamaliza kuuandaa kutokana na kuwa na majukumu ya kikazi.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya wakili wa utetezi, Kusalika Augostine kuwasilisha maombi mahakamani hapo akidai wateja wake wanahitaji kupata dhamana kwa sababu mashtaka yanayowakabili yanadhaminika.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo  ni Nyangi Mataro( 54) mwalimu wa shule ya  msingi Ufukoni na mkazi wa Kisiwani Mkajuni Kigamboni, mfanyabaishara, Farijia Ahmed (39) mkazi wa Soko Maziwa Kigamboni, Malaki Mathias b(39) mkazi wa Magogoni, Kristomsi Angelus (25) mkazi wa Soko Maziwa,  Fundi Ujenzi Pamfili Nkoronko (40) mkazi wa Tungi Kasirati na Hunry Fredrick (38) mkazi wa Tungi Kigamboni nq Audai Ismail

washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka matatu ya uhujumu uchumi kwa kujiunganishia isivyo halali bomba la mafuta ya  dizeli, kinyume cha sheria  ya Uhujumu uchumi.

Ilidaiwa katika tarehe tofauti kati ya mwaka 2015 hadi Januari 8, 2018 katika eneo la Tungi Muungano wilaya ya Kigamboni, washtakiwa kwa pamoja wanadaiwa kujiunganishia bomba la mafuta ya dizeli lenye upana wa inchi moja kutoa katika bomba lenye upana wa inchi 24, bila kuwa na kibali kutoka (TPA).

Inadaiwa walijiunganishia mafuta hayo kutoka katika bomba la rangi ya silva lenye upana wa inchi 24 ambalo halishiki kutu.

katika shtaka la kuharibu miundo mbinu, ilidaiwa,  kati ya mwaka 2015 hadi Januari 8, 2018 katika eneo la Tungi Muungano wilaya ya Kigamboni, washtakiwa walitoboa na kuharibu bomba la mafuta ya dizel lenye upana wa inchi 24, ambalo lilikuwa likitumika kufirisha mafuta,  mali ya (TPA).

Aidha washtakiwa kwa pamoja walitoboa na kuharibu bomba la mafuta mazito( Crude oil) lenye upana wa Inchi 28, ambalo lilikuwa likitumika kusafirisha mafuta ghafi, mali ya (TPA)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...