Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii

MKUU wa Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam Kisare Makori amehitimisha maadhimisho ya Wiki ya maji jijini yenye kauli mbiu ya Hifadhi Maji na Mifumo ya Ekolojia kwa Maendeleo ya Jamii.

Ametumia hitimisho la maadhimisho hayo kufungua mradi mdogo wa utakatishaji maji taka katika eneo ya Mburahati jijini.Akizungumza leo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Makori amesema maji yanayopatikana jijini kwa sasa ni asilimia 75 pekee na hadi kufikia mwaka 2020 maji yatapatikana kwa asilimia 95 na kufikia mwaka 2025 wakazi wote wa jiji watapata maji kwa asilimia 100.

Akizungumzia kuhusu mafanikio ya miradi maji Makori amesema miradi inayotekelezwa na DAWASA na DAWASCO katika mradi wa Ruvu chini ni lita milioni 270 kutoka lita milioni 182 zinazalishwa kwa siku na kuhudumia wakazi wa Bagamoyo, Kawe na maeneo ya jirani na mradi wa Ruvu juu lita 196 kutoka lita milioni 82 zinazalishwa kwa siku na kuhudumia wakazi wa maeneo ya Kibaha, Mbezi, Ubungo na maeneo ya jirani. 

Amesema zaidi ya visima 20 vimechimbwa na kunufaisha wakazi wa Kimbiji Mpera na maeneo yake.Amepongezwa wananchi kwa kukubali kuunganishwa na huduma ya maji kutoka laki 123,000 hadi kufikia 228,000.Pia amewataka wananchi kushiriki shughuli za usafi licha ya kuwa na asilimia 10 tu ya wakazi wanaopata huduma hiyo na amehaidi hadi kufikia 2020 asilimia 30 ya wakazi watafikiwa na huduma hiyo.

Makori amesema mwaka 2017 hadi mwaka 2020 miradi 50 ya uondoaji maji taka itajengwa Jangwani na kusaidia maeneo yenye wakazi wengi, mlipuko wa magonjwa na watu wenye kipato kidogo.

 Mkuu wa Wilaya ya Ubungo,Kisare Makori akizungumza katika  maadhimisho ya wiki ya maji jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo,Kisare Makori (alievaa kofia ya kijani) akipanda mti katika mradi wa kuchaata maji taka.
 Mkuu wa Wilaya ya Ubungo,Kisare Makori akiweka jiwe la msingi la ujenzi katika mradi wa kuchaata maji taka.
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo,Kisare Makori  aiwa ameambana na viongonzi mbalimbali wakigangua eneo la mradi huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...