Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma
Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB,  Dkt. Akinumwi  Adesina, amesema Benki hiyo imeridhishwa na utekelzaji wa miradi ya nishati hapa nchini kwani inachochea mageuzi katika maisha ya wananchi .
 Akizungumza mara baada ya kuwasili Mkoani Dodoma na kutembelea  kituo cha kupoza umeme cha Zuzu, mkoani Dodoma, amesema kuwa  benki hiyo inatambua na kupongeza juhudi za  Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika kusukuma mbele kurudumu la maendeleo.
Dkt. Adesina ameeleza kuwa ujenzi wa kituo hicho cha kupoza umeme ni mkakati wa Serikali ya Awamu ya Tano ya kuondoa changamoto ya upatikanaji wa nishati ya umeme kwa wananchi wake na umelenga pia kupunguza tatizo la upatikanaji wa umeme katika nchi jirani zinazopakana na Tanzania ikiwemo Burundi na Kenya.
Alisema kuwa katika kuhakikisha mpango huo wa kupeleka umeme huo na kuunganisha na nchi jirani, Benki yake imetoa kiasi cha dola za Marekani milioni 75 kufanikisha mradi huo wenye thamani ya zaidi ya dola milioni 220.
"Umeme ni jambo muhimu sana katika maendeleo ni sawa na damu katika mwili wa binadamu, ukiwa na damu mwilini unakuwa na hai kama huna unakufa! kwa hiyo uchumi bila umeme wa uhakika hauwezi kushamiri" alisisitiza Dkt. Adesina
Aliahidi kuwa Benki yake itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kukuza maendeleo ambapo hivi sasa Benki yake iko katika mazungumzo na Serikali ili mkopo nafuu wa dola za Marekani milioni 165 uweze kupatikana kwa ajili ya kujenga mradi wa nishati ya umeme katika ukanda wa Kaskazini Magharibi mwa nchi.
"Vile vile tutawasilisha kwenye Bodi ya Wakurugenzi wa Benki yetu ili kiasi cha dola za Marekani milioni 45 kinachoombwa na Serikali kwa ajili ya kujenga mradi wa umeme unaotokana na joto ardhi uweze kupatikana ili kuboresha na kuwa na umeme wa uhakika nchini kwa ajili ya kusukuma maendeleo ya viwanda nchini" alisema Dkt. Adesina
Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu akisalimiana na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina mara baada ya kuwasili mjini Dodoma ambapo alitembelea na kukagua mradi wa kituo cha kupoza umeme cha zuzu mkoani humo .
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdori Mpango ( Mb) akimuongoza Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina mara baada ya kuwasili mjini Dodoma ambapo alitembelea na kukagua mradi wa kituo cha kupoza umeme cha zuzu mkoani humo.
Rais wa wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina akisisisitiza jinsi Benki hiyo inavyoridhishwa na hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo upatikanaji wa nishati hali itakayochochea maendeleo.
Mhandisi Mkuu wa Kituo cha kupoza umeme cha Zuzu, Mkoani Dodoma Bw. Joseph Mongi akitoa maelezo kuhusu namna kituo hicho kinavyofanya kazi wakati wa ziara ya Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina katika kituo hicho.
Sehemu ya Miundombinu ya kituo cha kupoza umeme cha Zuzu kilichoko mkoani Dodoma kama inavyoonekana.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdori Mpango (Mb) na Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu, wakimuongoza Rais wa wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina kukagua miundombinu ya Kituo cha kupoza umeme cha Zuzu, mjini Dodoma.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano-Wizara ya Fedha na Mipango).


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...