Na Rhoda Ezekiel Kigoma

MKUU wa Wilaya ya Buhigwe Brigedia Jenerali Marko Gaguti amewapongeza vijana wa Kigoma kwa kitendo walichokifanya cha kuuenzi Muungano wa Tanzania, kwa kuandaa mchezo wa kirafiki baina ya vijana wa CCM na waendesha Bodaboda bila kujali itikadi za vyama vyao.

Pongezi hizo alizitoa jana baada ya mchezo huo uliofanyika Viwanja vya Kawawa Manispaa ya Kigoma Ujiji, wakati akitoa zawadi kwa washindi, ambapo vijana wa CCM waliibuka washindi kwa penati tano kwa nne dhidi ya timu ya vijana wa bodaboda.

Pia kila timu ilipata mbuzi mmoja na mchele kilo 20 kwa ajili ya kudumisha na kuuenzi Muungano ambapo Brigedia Gaguti amesema vijana hao ameonesha mfano mzuri wa kuigwa na wameienzi falsafa ya Muungano kwa kitendo walichokifanya na kuwataka waendeleee kuudumisha umoja na mshikamano hata katika maendeleo.

"Nitoe pongezi kwa vijana wa Kigoma, viongozi wa UVCCM na viongozi wa bodaboda kwani hili ambalo mmenlifanya ni jambo lenye tija na maana kwani mmedumisha na kuunzi Muungano kwa vitendo.Kwa upande wa Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Kigoma Silvia Sigura amesema wao kama viongozi wa vijana walibuni mchezo huo katika Sikuku ya Muungano na lengo ni kuwaunganisha vijana wa Mkoa wa Kigoma ili wawe wamoja na kuendeleza ushirikiano katika kuuinua Mkoa huo kiuchumi.


Amesema michezo ni afya lakini pia ni moja ya eneo ambalo linaunganisha vijana na watu wa rika mbalimbali na kutumia nafasi hiyo kusisitiza umuhimu wa vijana wa Kitanzania kuwa wazalendo kwa Taifa lao.Wakati huohuo baadhi ya vijana wa bodaboda ambao wameshiriki mchezo huo wametoa shukrani kwa uongozi wa UVCCM kwa kuandaa mpambano huo ambao msingi wake ni kudumisha muungano wetu kati ya Tanzania Bara na Zanzibar.
MKUU wa Wilaya ya Buhigwe Brigedia Jenerali Marko Gaguti akizungumza wakati akiwapongeza Vijana wa Kigoma kwa kuandaa mchezo wa kirafiki baina ya Vijana wa Chama cha Mapinduzi na Bodaboda bila kujali itikadi za Vyama vyao kwa dhana ya kuuenzi Muungano wa Tanzania, .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...