Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

Ujio wa ndege za serikali kutaongeza huduma ya usafiri wa anga,mapato ya serikali pamoja na wananchi kuona huduma ya usafiri wa anga sio anasa kama ilivyokuwa ikitafsiriwa na baadhi ya watu.

Hayo ameyesema leo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA),Richard Mayongela wakati akizungumza na Michuzi Media, amesema kuwa katika kwenda na uchumi wa viwanda ni lazima kuwepo kwa viwanja bora vya ndege katika kurahisisha usafiri mali ghafi pamoja na abiria.

Amesema kuwa viwanja vyote vya ndege vinaboreshwa kwa ajili ya kutoa huduma ya usafiri wa anga katika mikoa mbalimbali ambapo ndege zinazonunuliwa zitatumika katika safari za mikoa hiyo.Mayongela amesema kuwa fedha zinazotumika kujenga viwanja hivyo ni za watanzania kutokana na nguvu ya Rais Dk. John Pombe Magufuli kuweka mkazo katika ukarabati wa viwanja ili kuweza kutoa huduma bora katika usafiri.

“Mapinduzi ya Rais Dk. John Pombe Magufuli anayoyafanya katika sekta ya usafiri wa anga kwa kununua ndege baadhi ya watu hawawezi kujua faida lakini watajua baada ya muda mfupi kutokana na ajira katika viwanja vya ndege pamoja na usafirishaji wa haraka wa bidhaa ambazo zinaharibika kwa muda mfupi kwenda kuuza nje ya nchi”amesema Mayongela.

Amesema katika viwanja vya ndege watajenga sehemu za kuhifadhi bidhaa ambazo zinaharibika katika kipindi kifupi ikiwa ni kuwafanya wafanyabiashara kuwa na uhakika bidhaa hizo katika kusafirisha kwenda nje ya nchi kwa ajili soko.Kaimu Mkurugenzi Mkuu huyo amesema katika kipindi hiki hakuna kulala ikiwa nia ya kumsaidia Rais Dk. John Pombe Magufuli katika kuifikisha Tanzania katika uchumi wa kati wenye maisha bora ya watanzania.

“Kazi yetu mamlaka ni kusimamia huduma ya usafiri kwa kujenga viwanja vya kisasa ili ndege zinazotumia viwanja hivi viweze kusukuma maendeleo ya nchi yetu na kama watanzania tunayofanya kazi hizi kuacha alama kwa vizazi vya sasa na vijavyo” amesema Mayongela.Amesema ujenzi wa Rada ni moja ya kuhakikisha hali ya usalama wa usafiri wa anga ina kuwa kwa viwango vya kimataifa ambavyo vimeanishwa katika utoaji wa huduma za ndege.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Viwanja vya Ndege nchini (TAA), Richard Mayongela akizungumza na Michuzi Blog leo jijini Dar es Salaam kuhusiana na masuala mbalimbali katika usimamizi wa viwanja vya ndege nchini,(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii)
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Viwanja vya Ndege nchini (TAA), Richard Mayongela akizungumza na Michuzi Blog kuhusiana na masuala mbalimbali katika usimamizi wa viwanja vya ndege nchini, leo jijini Dar es Salaam.
Muonekano wa sehemu ya uwanja wa Ndege cha Mwalimu Julius Nyerere pamoja na ndege zikiwa katika uwanja huo .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...