Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
JAMII
imeaswa kujenga misingi imara ya malezi ya watoto ili wasiweze kuishi
maisha ya mitaani na ambayo yanasababisha kokosa haki za kupata elimu
pamoja na malezi mengine.
Hayo
ameyasema leo Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto, Sihaba Nkinga wakati akizindua ripoti ya Taifa ya
Watoto wanaoishi na kufanya Kazi Mitaani nchini Tanzania, amesema kuwa
sehemu salama ya kuishi watoto ni katika familia au jamii.
Amesema
kuwa katika ripoti hiyo watoto wa kike wamekuwa wakionekana katika
majira ya usiku wakijiuza huku watoto wakiume wanaonekana majira ya
mchana na usiku.
Nkinga
amesema kuwa serikali itafanyia kazi mapendekezo ya ripoti hiyo ili
katika kuweza kuhakikisha watoto hao wanakwenda katika familia zao.
Amesema
sababu zinazowafanya watoto kuishi na kufanya kazi mitaani ni
umasikini pamoja na ukatili wa kupindukia na kuamua baadhi ya watoto
kutoroka katika familia zao na kuingia mitaani.
“Jamii
iendelee kuishi kwa amani na misingi bora katika malezi ya watoto
katika kuhakikisha hawakimbilii mitaani kwa kuishi kwa kukosa chakula,
elimu pamoja wengine kupoteza maisha kutokana na kupigwa “amesema
Nkinga.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Sihaba Nkinga akizungumza wakati wa uzinduzi wa ripoti ya Taifa ya
Watoto wanaoishi na kufanya Kazi Mitaani nchini Tanzania uliofanyika leo
jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Sihaba Nkinga akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ripoti ya Taifa ya
Watoto wanaoishi na kufanya Kazi Mitaani nchini Tanzania uliofanyika leo
jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Railway Afrika, Peter Kent akizungumza na waandishi wa habari juu ya
mikakati ya shirika hilo katika masuala ya watoto wanaoishi na kufanya
kazi mitaani wakati wa uzinduzi wa ripoti ya Taifa ya Watoto wanaoishi
na kufanya Kazi Mitaani nchini Tanzania uliofanyika leo jijini Dar es
Salaam.
Naibu
Mwakilishi Mkazi USAID Kizazi Kipya Project wa PACT Tanzania, Levina
Kikoyo akizungumza jinsi ya utafiti waliofanya katika ripoti hiyo.
Sehemu
ya wadau mbalimbali wa masuala ya watoto waliohudguria katika uzinduzi
wa ripoti ya Taifa ya Watoto wanaoishi na kufanya Kazi Mitaani nchini
Tanzania uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Sihaba Nkinga akiwa na wawakilishi wa mashirika wakati wa uzinduzi ya
Taifa ya Watoto wanaoishi na kufanya Kazi Mitaani nchini Tanzania
uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...