Na Mdau wa blog ya jamii
Japokuwa mvua zinaendelea kunyesha, zikiwa zinaweza kuleta madhara makubwa katika barabara mbali mbali jijini Dar es Salaam na nchini kwa Ujumla lakini zipo barabara zinaweza kuokolewa iwapo watendaji husika watafanya kazi zao kwa weledi na bila kusukumwa na mamlaka za juu.

Napenda kutolea mfano barabara ya kutoka Tabata Mwananchi karibu kabisa na ofisi za gazeti la Mwananchi kuelekea Tabata Kisiwani, barabara hiyo imekatwa na maji yaliyoshindwa kupita katika matundu ya Daraja ambayo yameziba hiyo yakaamua kutafuta njia mbadala ya kupitia.

Matundu hayo hayajaziba leo wala jana, yemeziba tangu mvua za awali, na mvua hizo zilikuwa zikisimama hata kwa wiki moja lakini hakuna jitihada zilizochukuliwa na wahusika kuzibua matundu hayo ili kuruhusu maji yapite na kutokuharibu tena barabara.

Unaweza kujiuliza, hivi kipindi mvua zinasimama mamlaka husika hazioni umuhimu wa kuzibua milango ya daraja hilo?, Je hawaoni mateso tunayoyapata wakazi wa Tabata Kisiwani? Je hawajui kuwa kukosekana kwa mawasiliano kati ya wakazi wa Tabata Kisiwani na sehemu zingine ni hatari kubwa hata kwa wagonjwa na akina mama wajawazito pale inapotokea dharura? Je wanataka hadi kiongozi wa juu ili awape maelekezo? na kama wanajua je wanataka kupata nini baada hiyo barabara kuharibika?

Mvua ya leo ndio imekata kabisa barabara nakufanya magari yashindwe kupita huku ile barabara ya kutokea upande wa Tabata Kimanga nayo haipitiki kwakuwa Makalavati yaliyowekwa yameliwa na maji hiasi cha magari kushindwa kupita, kwa ujumla hali si shwari kabisa.

Naziomba mamlaka zinazohusika pamoja na uongozi wa Tabata Kisiwani kuliona hili kama dharura, ili wakazi wa Tabata kisiwani na sisi tujione kama watanzania huru na wenye kustahili kuhudumiwa na watu wenye kupata malipo yanayotokana na kodi zetu, pia naiomba ofisi ya Mkuu wa Mkoa kuingilia kati suala hili ili kunusuru maisha ya wanatabata Kisiwani ili dharura itakapotokea tuweze kujitete kwa haraka.
 Muonekano wa Daraja la Tabara Mwananchi kuelekea Tabara Kisiwani lililovyoathiriwa na mvua zinazoendelea kunyesha baada ya maji kushindwa kupita kwenye matundu ya daraja hilo na kupita juu.
Muonekano wa Barabara ya kuelekea Tabata Kisiwani kutoka Tabata Mwananchi maji yakiwa yamejaa barabarani baada ya maji wengi kushidwa kupita katika matundu ya daraja lililopo katika barabara hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...