JUMIA imekabidhi simu mbili za Samsung Galaxy S9 na S9+ kwa wateja wake wawili ambao waliibuka washindi kupitia zoezi la kusaka simu kwenye mtandao wao (Treasure Hunt) kupitia kampeni ya ‘Mobile Week.’

Katika zoezi hilo wateja waliofanikiwa kuzipata simu hizo zilizofichwa, walipewa ofa ya kuzinunua kwa bei ya chini kupindukia tofauti na gharama yake halisi. Baada ya kufanikiwa kufanikiwa kuipata simu ya Samsung Galaxy S9, mteja Happiness Keto aliinunua simu hiyo kwa shilingi 59,000 tu, wakati mwenzake Lumby Elia yeye aliinunua Samsung Galaxy S9+ kwa shilingi 81,000 pekee!

Bei halisi ya simu ya Samsung Galaxy S9 ni shilingi 2,049,000 ikiwa imepunguzwa kutoka shilingi 2,500,000 wakati Samsung Galaxy S9+ ni shilingi 2,315,000 nayo ikiwa imepunguzwa kutoka shilingi 2,800,000! Hivyo unaweza kujionea ni kwa namna gani wateja hawa walivyokuwa na bahati!

Simu hizi zilizinduliwa mapema mwezi Februari mwaka huu na kampuni ya Samsung duniani ambapo kwa hapa nchini Tanzania ilikuwa ikipatikana kwa malipo ya kabla kupitia kwenye mtandao wa Jumia pekee.Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa simu yake ya Samsung Galaxy S9+, Lumby Elia amesema kuwa ana furaha sana hatimaye kuishika simu hiyo mkononi kwa mara ya kwanza kwani ni kama ndoto kuinunua kwa bei hiyo kwa sababu ni sawa na bure.

“Ni ndoto ya watu wengi kumiliki bidhaa ambayo ni toleo jipya hususani kama simu ambazo kila mwaka huwa zinakuja na matoleo na maboresho tofauti. Simu hii kwangu mimi ni kama ndoto kutokana na ubora na thamani yake pamoja na uwezo ilionao,” alisema na kumalizia Bi. Elia, “Naishukuru sana Jumia kwa zawadi hii lakini pia kwa fursa iliyoitoa kwa wateja wake kuweza kutumia bidhaa halisi na mpya kabisa iliyoingia kwa mara ya kwanza sokoni. Nawasihi wateja wengine wakiona fursa kama hizi wasizipuuzie, ni kweli kama hivi mnavyoona.”

Mkurugenzi Mkuu wa Jumia Tanzania, Bw. Zadok Prescott , akimkabidhi simu ya Samsung Galaxy S9, mteja Happiness Keto aliyoinunua simu hiyo kwa shilingi 59,000 tu katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi Mkuu wa Jumia Tanzania, Bw. Zadok Prescott , akimkabidhi simu ya mwakilishi wa mteja wa Lumby Elia aliyoinunua simu hiyo aina ya Samsung Galaxy S9+ kwa shilingi 81,000 pekee!
Meneja Uhusiano wa Umma wa Jumia Tanzania, Kijanga Geofrey, akizungumza kwenye mkutano huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...