Mkuu wa wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro ambaye pia ni mgeni rasmi katika uzinduzi wa kituo cha msaada wa kisheria Mohamed Utaly akikata utepe katika vitabu vinavyozungumzia mambo ya sheria kuashiria uzinduzi wa kuanzishwa kwa kituo cha msaada wa kisheria chuo kikuu Mzumbe Mkoani Morogoro,kulia ni Makamu Mkuu wa chuo kikuu cha mzumbe Prof, Lughano Kusiluka .
Mkuu wa kitivo cha sheria chuo kikuu cha mzumbe Prof, syriacus Binamungu akimkaidhi Makamu Mkuu wa chuo Kikuu cha Mzumbe mkoani Morogoro Prof, Lughano Kusiluka vitabu vinavyohusu mambo ya sheria kwa ajili ya makamu Mkuu wa chuo kukabidhi  kwa mgenia rasmi ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Mvomero Mohamed Utaly ili aweze kuzindua rasmi. Makamu mkuu wa chuo kikuu cha Mzumbe mkoani Morogoro Prof Lughano Kusiluka akiwasisitizia wanchuo kitivo cha sheria kuhakikisha wanajituma kutoa msaada wa kisheria kwa wananchi mara baada ya kuzinduliwa kwa kituo hicho chuoni hapo .
Mhadhiri msaidizi chuo kikuu mzumbe Hassani Ramadhani Gyunda (aliyevaa shati nyeupe) akimuelezea mgeni rasmi Mohamed Utaly (kushoto) jinsi watakavyoweza kufanya kazi katika kutatua changamoto za kisheria ambazo zinawakabili wananchi, aliyekaa chini upande wa mgeni rasmi ni mwananchi anayepatiwa msaada wa kisheria Rashidi Ramadhan mkazi wa sangasanga mkoani Morogoro .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...