SERIKALI imewaasa viongozi wa dini waeuepuke migogoro ya mara kwa mara katika Makanisa yao na badala yake waendelee kuwajenga waumini wao wakue kiroho na kujenga dhana ya umoja na upendo katika Taifa.
Pia imesema inawashukuru viongozi wa dini na madhehebu yote ya dini kwa kuendelea kuiombea nchi amani, mshikamano na utulivu, jambo ambalo linaongeza chachu kubwa kufikia mafanikio ya maendeleo ya kijamii, kisiasa na kiuchumi.
Hayo yamesemwa leo (Jumapili, Mei 20, 2018) na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika ibada ya kutawazwa Askofu Dkt. Maimbo Mndolwa wa Dayosisi ya Tanga kuwa Askofu Mkuu wa saba wa Kanisa la Anglikana Tanzania. Ibada hiyo imefanyika katika Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu Dayosisi ya Central Tanganyika Jijini Dodoma.
“Nawaombeni wote kwa ujumla wetu, tuendelee kutumia Makanisa yetu kuombea Taifa hili ili tuendelee kuishi kwa amani, upendo na mshikamano”. Watu wa Mungu ni watu wa Upendo, watu wa Mungu ni watu wa amani, watu wa Mungu ni watu wa kiroho”.
Waziri Mkuu ameongeza kuwa “haitarajiwi kuona watu wa Mungu wakiwa katika mstari wa mbele kuchochea migogoro, kuvunja amani ya Kanisa na kuongoza makundi yanayopingana katika kazi ya Bwana”.Amesema jukumu la makanisa ni kuwajenga waumini kukua kiroho, na kazi ya kuwaongoza watu wamjue Mwenyezi Mungu, ambapo amewaomba imani yao iwe moja na matendo yao yafanane na yale ya Kristo Yesu wanayemuamini.
Waziri Mkuu amesema kuwa nchi haiwezi kupata mafanikio ya kiuchumi na kijamii bila kuilinda amani iliyopo, hivyo amewaomba warejee kumbusho la maandiko Matakatifu katika Waebrania 12:14 “Tatufeni kwa bidii kuwa na Amani na watu wote”.
Pia Waziri Mkuu ametoa wito kwa viongozi hao na wananchi kwa ujumla waendelee kuwaombea viongozi wa Tanzania hususani Rais Dkt. John Magufuli, kuendelea kuwa na afya njema, busara, upendo, hekima katika kuiongoza nchi yetu.
Waziri Mkuu ambaye amemuwakilisha Rais Dkt. Magufuli katika ibada hiyo amesema Serikali inatambua ushirikiano uliopo kati ya madhehebu mbalimbali ya dini nchini kwa ujumla wake na kwamba ushirikiano huo ni wa kihistoria.
Askofu
Mkuu wa saba wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Maimbo Fabian
Mndolwa akila kiapo wakati alipotawazwa kuw Askofu Mkuu wa Kanisa la
Anglikana Tanzania, jijini Dodoma, Mei 20, 2018. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kasim Majaliwa akisalimiana na Askofu Mkuu Mstaafu wa Kanisa la
Anglikan Tanzania, Jaco Chimeldya katika sherehe ya kumtawaza Askofu
Mkuu wa Saba wa kanisa hilo, Maimbo Fabian Mdolwa jijini Dodoma, Mei
20,2018. Mheshimiwa Majaliwa alimwakilisha Rais John Pombe Magufuli
katika sherehe hiyo.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa, akizungumza katika Rais John Pombe Magufuli
kwenye sherehe ya kumtawaza Askofu Mkuu wa saba, Maimbo Fabian Mndolwa,
jijini Dodoma, Mei 20, 2018.2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Askofu Mkuu wa saba wa Kanisa la
Anglikana Tanzania, Maimbo Fabian Mndolwa baada ya Askofu huyo
kutawazwa kuwa Askofu Mkuu wa Kanisa hilo, jijini Dodoma, Mei 20, 2018,
kulia ni mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa. Waziri Mkuu
alimwakilisha Rais John Pombe Magufuli.
Spika
wa Bunge Job Ndugai akisalimiana na Askofu Mkuu Mstaafu wa Kanisa la
Anglikana Tanzania , Oscar Mnunga katika sherehe ya kumtawaza
Askofu Mkuu wa Saba wa kanisa hilo, Maimbo Fabian Mndolwa jijini
Dodoma, Mei 20, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...