Na Mwandishi wetu,
SERIKALI imeombwa ifikirie kutoa ruzuku kwa radio za jamii kupitia Mtandao wa Asasi ya Habari za Maendeleo (TADIO) ili waweze kuandika habari ya mambo yanayojiri vijijini badala ya kutegemea habari za matukio.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa TADIO, Prosper Kwigizewakati wa mkutano mkuu wa mtandao huo uliosajiliwa mwaka jana na msajili wa mashirika ya kiraia na kuhudumu kwa takribani radio zote za jamii nchini.
Alisema kwa sasa wanajivunia kuhudumia watu takaribani milioni 35 lakini wana shida kubwa ya kuweza kuandika habari za maendeleo vijijini kutokana na tatizo la fedha.
Alisema wao kama radio za jamii zinasikilizwa vyema katika maeneo yao kwa kuwa wanaandika habari za wananchi wa huko katika ngazi ya mtaa na kijiji na kama mabadiliko yanatakiwa kufanywa katika nchi wao ndio wanaoweza kuwa chachu.
 Hata hivyo alisema pamoja na kuwa karibu na wananchi wanalazimika kuandika zaidi habari za matukio kutokana na kukosa fedha za kutuma waandishi vijijini kupiga kambi kwa ajili ya habari za uchunguzi ambazo zitaibua masuala mbalimbali.
Alisema pamoja na kupata msaada mkubwa kutoka mataifa ya Sweden na Uswis kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi Elimu na Utamaduni (UNESCO), msaada wao hautoshi na hivyo kuitaka serikali na wadau wa ndani kama Mifuko ya Hifadhi kuwezesha radio hizo kusimama zenyewe kimapato na kitendaji.
Alisema kuna masuala mengi ya vijijini katika mikoa ya pembeni ambayo radio hizo zikiwezesha zinaweza kusaidia kujulisha taasisi nyingine nini kinajiri na nini kinastahili kufanywa.
 Mwenyekiti wa Mtandao wa Asasi ya Habari za Maendeleo (TADIO), Prosper Kiwigize akifungua mkutano mkuu wa mtandao huo uliofanyika katika ukumbi wa Kato jijini Dodoma. Kulia ni Katibu wa Mtandao huo, Marko Mipawa, Afisa Miradi kwenye Kitengo cha Mawasiliano na Habari kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi Elimu na Utamaduni (UNESCO), Rose Mwalongo (wa pili kushoto), pamoja na Mkurugenzi wa MISA-TAN, Gasirigwa Sengiyumva (kushoto).
 Mwenyekiti wa Mtandao wa Asasi ya Habari za Maendeleo (TADIO), Prosper Kiwigize akionyesha cheti cha usajili wa Mtandao wa Asasi ya Habari za Maendeleo (TADIO) unaohusisha Tanzania bara na Visiwani wakati wa mkutano mkuu wa mtandao huo uliofanyika katika ukumbi wa Kato jijini Dodoma.
 Afisa Miradi kwenye Kitengo cha Mawasiliano na Habari kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi Elimu na Utamaduni (UNESCO), Rose Mwalongo akizungumza wakati wa mkutano mkuu wa Mtandao wa Asasi ya Habari za Maendeleo (TADIO) uliofanyika katika ukumbi wa Kato jijini Dodoma.
 Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Habari Unesco nchini, Nancy Kaizilege akitoa salamu kwa wajumbe ambapo ameahidi kuendeleza ushirikiano na TADIO wakati wa mkutano mkuu wa Mtandao wa Asasi ya Habari za Maendeleo (TADIO) uliofanyika katika ukumbi wa Kato jijini Dodoma.
 Katibu wa Mtandao wa Asasi ya Habari za Maendeleo (TADIO), Marco Mipawa akisoma ripoti ya mapato na matumizi kwa kipindi cha Januari 2017 mpaka Mei 2018 pamoja na taarifa ya bodi ya TADIO ya utekelezaji kwa kipindi cha Julai 28, 2017 mpaka Mei 3, 2018 wakati wa mkutano mkuu wa mtandao huo uliofanyika katika ukumbi wa Kato jijini Dodoma.
 Mkurugenzi wa MISA-TAN, Gasirigwa Sengiyumva akizungumza na wajumbe wakati wa mkutano mkuu wa Mtandao wa Asasi ya Habari za Maendeleo (TADIO) uliofanyika katika ukumbi wa Kato jijini Dodoma.
 Mjumbe wa TADIO kutoka Kahama FM, Maria Lembeli akichangia maoni wakati wa mkutano mkuu wa mtandao huo uliofanyika katika ukumbi wa Kato jijini Dodoma.
 Mjumbe wa TADIO kutoka redio Orkonerei FM, Baraka Ole Maika akiuliza swali na kuchangia maoni wakati wa mkutano mkuu wa mtandao huo uliofanyika katika ukumbi wa Kato jijini Dodoma.
Wajumbe wa Bodi ya Mtandao wa Asasi ya Habari za Maendeleo (TADIO) katika picha ya pamoja baada kumaliza mkutano mkuu wa mtandao huo uliofanyika katika ukumbi wa Kato jijini Dodoma.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...