Kurugenzi CUP ’18 yazidi kutimua vumbi katika dimba la shule ya msingi
Haydom Wilayani Mbulu Mkoani Manyara, kwa timu ya Rema 1000 FC kwa
kuigaragaza pasipo huruma timu ya Lambo FC kwa mabao 5-3.

Katika mchezo huo uliofanyika leo alasiri timu hizo zilitoana jasho,
upinzani mkali, katika kulisakata kabumbu na kuonyeshana ufundi,
kwenye mashindano hayo  yaliyoandaliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya wilaya ya Mbulu, Hudson Kamoga.

Bao la kwanza la timu ya Rema 1000 FC lilitiwa kimiani na winga
machachari wao Shafii Said wenye dakika ya 26 ya kipindi cha kwanza
cha mchezo huo.

Mshambuliaji hatari wa timu ya Rema 1000 FC Masudi Juma aliipatia timu
yake bao la pili kwenye dakika ya 29 mara baada ya kuwachambua pasipo
na huruma walinzi watatu wa timu pinzani na kupachika kimiani bao la
kiufundi, hadi mapumziko timu ya Lambo haikuona nyavu ya timu pinzani.

Kipindi cha pili timu ya Lambo FC kupitia kocha wake ilifanya
mabadiliko kwa kuwatoa washambuliaji wawili na kuingiza nguvu mpya
ambayo ilibadilisha sura ya mcheo na kuleta maajabu kwenye viwanja
hivyo kwa kurudisha mabao mawili na kuongeza la tatu.

Mchezaji Godfrey Ernest wa timu ya Rema 1000 FC ya Haydom Manyara akimtoka mchezaji wa timu ya Rambo FC pia ya Haydom katika mchezo wao uliofanyika leo kwenye uwanja wa shule ya Msingi Haydom katika Mashindano ya  kombe la Kurugenzi Cup 2018 yaliyoandaliwa na Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu ambapo timu ya Rema 1000 FC imeibuka na ushindi wa Magoli 5-3 dhindi ya Rambo FC.
 Wachezaji wa timu ya Rema 100 FC ya Haydom wakishingilia  mara baada ya mchezaji Raurenc Marco kuifungia timu yake ya Rema 1000 FC goli lao la tano katika mchezo huo uliokuwa mkali dakika zote za mchezo.
 Kikosi cha timu ya Rema 1000 FC kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo huo.
 Kikosi cha timu ya Rambo FC kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo huo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...