Na Hamza Temba-WMU-Dodoma
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk.
Hamisi Kigwangalla amemteua mshindi wa taji la Miss Journalism Tanzania, 2018,
Witness Teddy Kavumo (21) kuwa balozi wa utalii wa Pori la Akiba Selous.
Amefanya uteuzi huo mwishoni mwa wiki
Jijini Dodoma baada ya mazungumzo na mwanamitindo huyo aliyemtembelea ofisini
kwake kwa ajili ya kuomba ufadhili wa kuandaa mradi wa kijamii ambao ni
sehemu ya shindano atakaloshiriki la taji la Dunia la Miss Journalism 2018
litakalofanyika Oktoba 27 Jijini Arusha.
Kufuatia uteuzi huo, Dk. Kigwangalla
amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania, Devotha Mdachi kuandika
barua ya uteuzi kwa balozi huyo mpya sambamba na kumkabidhi hati ya uteuzi ili
pamoja na mambo mengine aweze kunadi vivutio vya utalii vya pori hilo.
Wakati huo huo, Dk. Kigwangalla
amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania
TAWA, Dk. James Wakibara kuandaa safari maalum ya balozi huyo mteule aweze
kutembelea Pori la Akiba Selous kwa ajili ya kuona na kujifunza mambo mbalimbali
yanayohusu hifadhi hiyo kwa ajili ya utangazaji.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na Miss Journalism Tanzania, 2018, Witness Teddy Kavumo (21) ambaye pia ni mshindi wa mwaka jana wa mataji manne ya Uanamitindo nchini Afrika ya Kusini, alipomtembelea ofisini kwake Jijini Dodoma mwishoni mwa wiki kwa ajili ya kuomba ufadhili wa kushiriki mashindano ya Dunia ya Miss Journalism yatakayofanyika Jijini Arusha mwezi Oktoba mwaka huu. Aidha, amemteua mwanamitindo huyo kuwa balozi wa utalii wa Pori la Akiba Selous.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi
Kigwangalla akionyeshwa taji la urembo la "Miss Garden Route South Africa
2017" ambalo ni maalum kwa ajili ya kuhamasisha utalii nchini Afrika ya
Kusini na Miss Journalism Tanzania 2018, Witness Teddy Kavumo (21) aliyeshinda
taji hilo na mataji mengine matatu nchini humo mwaka jana, alipomtembelea
ofisini kwake mwishoni mwa wiki kwa ajili ya kuomba ufadhili wa kushiriki
kwenye mashindano ya Dunia ya Miss Journalism yatakayofanyika Jijini Arusha
mwezi Oktoba mwaka huu. Aidha, amemteua mwanamitindo huyo kuwa balozi wa
vivutio vya utalii vya Pori la Akiba Selous.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi
Kigwangalla akiwa kwenye picha ya pamoja na Miss Journalism Tanzania, 2018,
Witness Teddy Kavumo (21) ambaye pia ni mshindi wa mwaka jana wa mataji manne
ya Uanamitindo nchini Afrika ya Kusini, alipomtembelea ofisini kwake Jijini
Dodoma mwishoni mwa wiki kwa ajili ya kuomba ufadhili wa kushiriki mashindano
ya Dunia Miss Journalism yatakayofanyika Jinini Arusha mwezi Oktoba mwaka huu. Aidha,
amemteua mwanamitindo huyo kuwa balozi wa vivutio vya utalii vya Pori la Akiba
Selous.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi
Kigwangalla akiagana na Miss Journalism Tanzania, 2018, Witness Teddy Kavumo
(21) ambaye pia ni mshindi wa mwaka jana wa mataji manne ya Uanamitindo nchini
Afrika ya Kusini, baada ya mazungumzo ofisini kwake Jijini Dodoma alipomtembelea
mwishoni mwa wiki kwa ajili ya kuomba ufadhili wa kushiriki mashindano ya Dunia
ya Miss Journalism yatakayofanyika Jinini Arusha mwezi Oktoba mwaka huu. Aidha,
amemteua mwanamitindo huyo kuwa balozi wa wa utalii wa Pori la Akiba Selous.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...