JAMII inayojitambua ndiyo inayoweza kutumika katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Aidha kushindikana kwa mipango mingi ya udhibiti wa uharibifu wa mazingira kunatokana na uelewa duni na mipangilio isiyozingatia mahitaji halisi ya wananchi wa maeneo husika.

Kauli hiyo imo katika Mdahalo wa Kitaifa wa Kilimo cha kisasa kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika katika ofisi za ESRF.Katika mdahalo huo uliowezeshwa na Shirika la Kimataifa la Care kwa kushirikiana na taasisi ya FANRPAN na ESRF imeelezwa kuwa kuna changamoto kubwa kwa maendeleo ya kilimo na ukuaji wake kutokana na n chi nyingi Kusini mwa Afrika kutegemea mvua.

Aidha ilielezwa kuwa changamoto nyingine ni umaskini uliokithiri, upungufu nmkubwa wa raslimali watu, maandalizi hafifu ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na miundombinu dhaifu.Mmoja wa watoa mada kutoka Taasisi ya CARE International nchini Malawi, Vitumbo Chinoko alisema kwamba kumekuwa na kulegalega kwa matumizi ya teknolojia katika kusaidia kuhifadhi mazingira miongoni mwa wananchi na uwezeshaji kwa watendaji kiasi cha kuharibu muitikio unaonekana wakati wa mafunzo.

Chinoko alisema kwamba kutokana na hali hiyo walibuni kanuni ambazo wao wanaziita SUPER kanuni ambazo zikifuatwa vyema zinajibu matatizo yaliyopo sasa. Alisema kwamba Super ni mfumo wa uchakataji wa taarifa na utekelezaji wake unaolenga kuwafikia wananchi wa pembezoni ambao ndio washiriki wakubwa wa utunzaji wa mazingira na uzalishaji wa chakula.

Alisema kwa kutumia kanuni hizo wananchi wanaweza kutambua mwendelezo wa rasilimali ardhi na misitu waliyonayo, wakawezesha kuitumia kwa faida kutokana na uadimu wake.Aidha kanuni hizo zinahitaji mipango kuzingatia usawa wa kijinsia ili kuteketeleza sera katika uchumi.

Alisema mfumo wa masoko unazungumzwa ikiwa ni pamoja na ushiriki wa sekta binafsi katika kilimo ili kuipaisha na kuifanya kuwa na tija zaidi.Alisema kwa sasa kuna tatizo kubwa sana la kuwasilisha taarifa huku watengeneza sera wakiwa pekee yao bila kushirikisha wananchi ambao ndio watendaji wenyewe.

Mshehereshaji wa Mdahalo wa Kitaifa wa Kilimo cha kisasa kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi, Mtafiti mshiriki wa ESRF, Abdallah Henku akitoa utambulisho wa wanenaji wa mdahalo huo uliofanyika jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano wa ESRF.

Mkuu wa kitengo cha Uwezeshaji na Utawala Bora wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Danford Sango akitoa neno la ukaribisho kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dkt. Tausi Kida wakati wa Mdahalo  wa Kitaifa wa Kilimo cha kisasa kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Idara ya Menejimenti ya Mazingira Wizara ya Kilimo Bi. Shakwaanande Natai akiwasilisha mada kuhusu utekelezaji wa sera ya kilimo kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi wakati wa Mdahalo wa Kitaifa wa Kilimo cha Kisasa kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Muwasilishaji mada kutoka Taasisi ya CARE International nchini Malawi, Vitumbo Chinoko (wa pili kushoto) akifafanua kanuni za kufauta katika kuhifadhi mazingira na kilimo kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi wakati wa mdahalo wa kitaifa wa kilimo cha kisasa kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam. Wengine ni Mkuu wa Idara ya Tafiti zilizoanishwa ESRF, Bi. Vivian Kazi (kulia), Mkurugenzi wa Sera, Mawasiliano na Uragibishi FANRPAN, Francis Hale (wa tatu kulia), Meneja ushirikiano, uragibishi wa sera kutoka taasisi ya Food, Agriculture and Natural Resources Policy Analysis Network (FANRPAN) Bw. Lufingo Mwamakamba (wan ne kulia) pamoja na Mkuu wa kitengo cha Uwezeshaji na Utawala Bora wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Danford Sango (kushoto)  akimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dkt. Tausi Kida.
Mkurugenzi wa Sera, Mawasiliano na Uragibishi FANRPAN, Francis Hale akifafanua jambo wakati majadiliano kwenye mdahalo wa kitaifa wa kilimo cha kisasa kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...