Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewashauri hospitali ya CCBRT kufikisha ujumbe wa Fistula katika kila wilaya hapa nchini hata kwa kutumia radio jamii. 

Makamu wa Rais amesema hayo leo alipofanya ziara katika hospitali hiyo iliyopo Msasani jijini Dar Es Salaam. Makamu wa Rais amesema inasikitisha kuona asilimia kubwa ya wagonjwa wa Fistula ni wasichana wadogo.

Makamu wa Rais ameipongeza Hospitali ya CCBRT kwa kazi nzuri wanayoifanya kwa kutoa huduma nzuri kwa wagonjwa wote. Hospitali ya CCBRT ina miaka 25 kwenye huduma na imekuwa msaada mkubwa kwa wagonjwa kutoka makundi maalum kwa mfano: walemavu, wasioona, viziwi na sasa inapokea wagonjwa zaidi ya wagonjwa700 kwa siku.

Makamu wa Rais ametoa wito kwa CCBRT na Serikali kuelekeza nguvu kwenye kuzuia kwa kutoa elimu ili wasichana wajue na waelewe elimu ya uzazi na kuwawezesha. Mwisho, Makamu wa Rais alitoa shukrani kwa kazi kubwa inayofanywa na hospitali ya CCBRT hapa nchini na kuahidi kuendelea kuwa Balozi wa Fistula.

Mapema kabla ya kumkaribisha Makamu wa Rais Kuhutubia, Waziri wa ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu alisema anaipongeza CCBRT kwa kutoa huduma bila faida na kusema wapo kwenye mpango wa kufanya mazungumzo yatakayoiwezesha CCBRT kuwa kituo kikuu cha kutoa huduma kwa wagonjwa wa Fistula nchini.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimu baadhi ya watoto walioletwa kwa matibabu katika hospitali ya CCBRT kama wagonjwa wa nje,kulia anayetoa maelezo ni Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa CCBRT Bw. Erwin Telemans. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Bibi Helena Mjinja mwenye umri wa miaka 64 kutoka Musoma anayepata matibabu ya Fistula katika hospitali ya CCBRT jijini Dar es Salaam. (Picha na ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wanawake ambao wamepata matibabu ya Fistula na kupona na kisha kufundishwa kazi za mikono katika hospitali ya CCBRT jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Hospitali ya CCBRT Bw.Erwin Telemans juu ya utengenezaji wa viungo bandia vinavyotengenezwa kwa utaalamu wa hali ya juu katika hospitali ya CCBRT jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia watoto Mussa Hussein (kulia) mwenye umri wa miaka 8 mkazi wa Kigamboni na Abdul Hamad (kushoto) mwenye umri wa miaka 10 mkazi wa Yombo Vituka wakicheza mpira kwa kutumia miguu maalum, Makamu wa Rais leo alifanya ziara kwenye hospitali ya CCBRT jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...