NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ameamuru kuwekwa ndani wakandarasi wanaotekelezwa mradi wa maji yenye thamani ya zaidi ya bilioni tatu eneo la mkata wilayani Handeni baada ya kushindwa kuwepo kwenye eneo la mradi licha ya kupewa taarifa za uwepo wa ziara yake. 

Wakandarasi ambao walilazimika kuwekwa ndani ni Mkandarasi wa Kampuni ya Tansino Logistick Limited ya Dar Abdul Ismail na Charles Stephano ambaye ni mkandarasi wa ujenzi huku Chales Tarimbo mshauri Mkandarasi naye akikumbana na kadhia hiyo. 

Agizo hilo alilitoa leo wakati wa ziara yake ya kutembelea na kukagua miradi ya maji inayotekelezwa kwenye kata ya Mkata wilayani Handeni ambapo miradi hiyo mitatu ilikuwa ikigharimu zaidi ya sh.bilioni tatu. 

Akiwa kwenye eneo hilo Naibu Waziri huyo alisema haiwezekani wabunge wanaomba miradi ya maji na serikali inatenga lakini watu wachache wanatumia fedha hizo kwenye matumizi kwa maslahi yao binafasi na kuwafanya wananchi kuendelea kuteseka na tatizo la maji. 

Alisema kutokana na kuwepo kwa tabia hiyo ambayo imekuwa ikirudisha nyuma juhudi kubwa zinazofanywa serikali hawatavumiliwa badala yake watahakikisha wanachukuliwa hatua kali za kisheria ili kuweza kukomesha vitendo vya namna hiyo kwenye jamii. 
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso kulia akimsikiliza kwa umakini Mkuu wa wilaya ya Handeni Godwin Gondwe mara baada ya kutembelea mradi wa Maji eneo la Mkata katikati ni Mkurugenzi wa Mtendaji wa wilaya ya Handeni William Makufwe
 Wakandarasi ambao Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso aliotaka wawekwe ndani wakiwa chini ya ulinzi 
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso wa pili kutoka kushoto akiwa na Mkuu wa wilaya ya Handeni kulia wakati wakitembelea miradi ya maji wilayani humo wakati wa ziara yake kulia ni Mkurugenzi wa Mtendaji wa wilaya ya Handeni William Makufwe kushoto ni Diwani wa Kata ya Mkata
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso akiwa amepanda juu kwenye tenki eneo la mkata kulikagua wakati wa ziara yake,kulia kwake ni Mkuu wa wilaya ya Handeni Godwin Gondwe 
Mkurugenzi wa Mtendaji wa wilaya ya Handeni William Makufwe akimueleza jambo Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso mara baada ya kutembelea miradi ya maji kwenye eneo la Mkata katikati ni Mkuu wa wilaya ya Handeni Godwin Gondwe akifuatilia kwa umakini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...