Na Shushu Joel, Bariadi
Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya mama na Mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto  Ummy Mwalimu Jana mara baada ya kukagua ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje(OPD)  la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu, ambapo ameridhishwa na ujenzi wa jengo hilo.

Waziri Ummy amewahakikishia viongozi wa mkoa wa Simiyu kuwa Serikali imetenga shilingi Bilioni 1.5 na wadau wengine wameahidi kutoa shilingi bilioni 1.1 kwa ajili ya kukamilisha wodi ya mama na mtoto mkoani humo ili kupunguza hadha ya kuwachanganya watoto na wakubwa kipindi wanapokwenda kupata matibabu.

“Simiyu katika bajeti ya Serikali imetengewa shilingi bilioni 1.5 lakini tumepata pia shilingi bilioni 1.1 kutoka kwa wafadhili kwa ajili ya ujenzi waWodi ya mama na mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu, lengo letu ni kukamilisha ujenzi haraka ili tuiwezeshe Halmashauri ya Mji wa Bariadi, kuchukua majengo ambayo yanatumika sasa hivi kama Hospitali Teule ya mkoa” alisema Ummy.

Katika hatua nyingine Waziri Ummy alisema baada ya kukamilisha ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Serikali ina mpango wa kujenga Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Ziwa Mashariki Mkoani Simiyu, itakayohudumia mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga  ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Rufaa ya Bugando ambayo inahudumia mikoa takribani minane.


 Meneja wa Wakala wa Majengo nchini(TBA) Mkoa wa Simiyu Mhandisi Likimaitare Naunga (wa pili kulia) akimuonesha Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu(katikati) ramani ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, mara baada ya Waziri Ummy kutembelea na kuona maendeleo ya Ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa Nje(OPD) la hospitali hiyo Mjini Bariadi.
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka akimuongoza  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto. Ummy Mwalimu , wakati alipotembelea  na kuona maendeleo ya Ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa Nje(OPD) la hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu Mjini Bariadi.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akisaini kitabu cha wageni  wakati alipotembelea  na kuona maendeleo ya Ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa Nje(OPD) la hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu Mjini Bariadi.
 Waziri wa afya jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu sambamba na kaimu mkurugenzi wa Amref helth Africa Dr Aisa Mmmuya kulia akishuhudia tukio hilo la uzinduzi huo.
Waziri wa afya Ummy Mwalimu sambamba na mbunge wa Itilima Njalu Silanga wakielekea kuzindua mradi wa tuwatumikie.
                                (PICHA ZOTE NA SHUSHU JOEL)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...