CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimezindua rasmi kampeni za uchaguzi mdogo Kata ya Mawenzi ilipo Moshi Mjini huku kikitumia nafasi hiyo kuahidi kuenddelea kusimamia na kutoa fursa nyingi zaidi za maendeleo kwa wananchi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo wa kampeni hizo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole amesisitiza CCM kuendelea kusimamia na kutoa fursa nyingi zaidi za kimaendeleo kwa wananchi wa Moshi Mjini katika Kata ya Mawenzi.

Polepole amewaomba wananchi wa Kata ya Mawenzi kumpatia kura za ushindi mgombea wa CCM Apaikunda Ayo Naburi kuwa Diwani wa Kata hiyo ili awe kiungo cha fursa zitokanazo na Serikali ya CCM kwa wananchi wake.

Akifafanua kuhusu fursa hizo za wananchi Polepole amesema CCM imejipanga kuhakikisha wananchi wanapata mikopo ya Halmashauri bila usumbufu, mizengwe wala riba.

Pia wafanyabiashara wadogo wadogo waendelee kufanya shughuli zao kwa utaratibu mzuri pasina usumbufu na Vijana wa bodaboda na bajaji watazamwe katika jicho la utu, usawa na haki katika shughuli zao za usafirishaji wa abiria katikati ya mji wa Moshi.

"Naomba mtupatie Apaikunda awe jicho letu, mtu tunaye muamini, ndio kiungo akisema nasi tunatoa maelekezo kwa manufaa ya wananchi," amesema Polepole.

Uzinduzi huo wa kampeni, ni muendelezo wa mikutano ya kampeni ya uchaguzi Mdogo katika kata na majimbo ambapo CCM inaendelea kunadi Sera zake bora kwa wananchi.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole  akiwahutubia Wananchi na wafuasi wa chama hicho wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo,
amesisitiza CCM kuendelea kusimamia na kutoa fursa nyingi zaidi za kimaendeleo kwa wananchi wa Moshi Mjini katika Kata ya Mawenzi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...