Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

UTAFITI uliofanywa na Chuo Kiku cha Sokoine (SUA) umeonesha kuwa katika kila hekta moja ya shamba la mpunga la umwagiliaji hupoteza gunia tisa za mpunga kutokana na kushambuliwa na panya.

Kwa mujibu wa SUA utafiti huo ulianza kufanyika mwaka 2015 baada ya chuo hicho kupata malalamiko mengi kutoka kwa wakulima wa zao la mpunga ambao walidai kuwa panya ndio adui yao mkubwa.

Akizungumzia utafiti huo jijini Dar es Salaam Profesa Loth Mulungu ambaye ni Mtafiti Mdhibiti wa viumbe hai na uharibifu amesema kutokana na utafiti huo hivi sasa tayari wamegundua vizuizi na mitego ambayo ni sumu kubwa kwa panya wanaokula mipunga katika mashamba.

Akifafanua zaidi kwenye Maonyesho ya 13 Vyuo Vikuu ya Elimu ya Juu Tanzania (TCU) yanayofanyika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam Profesa Mulungu wanatumia vizuizi na mitego kwa ajili ya kuwakamata panya wanaoshambulia mpunga ambao tayari ulishakomaa katika shamba.

"Kwa siku tunatega panya zaidi ya mia mbili ambao hao wangekuwa wameingia kwenye shamba la mpunga wangekuwa wameshambilia zaidi mpunga ambao uliokuwa unasubiriwa kuvunwa,"amesema Profesa Malungu.

Pia amesema lengo lao kubwa ni kuongeza ufanisi katika uthibiti wa panya kwenye mashamba ya umwagiliaji na kwamba wadudu wengi waharibifu wakiwemo panya wanapenda kuvamia katika mashamba ya umwagiliaji kwa sababu mwaka mzima mashamba hayo yana mazao tofauti na yale mashamba yanayotegemea mvua za masika.

Hata hivyo amesema katika nchi ya Asia tayari wamefanikiwa kwa kutumia njia ya kuweka vizuizi na mitego katika mashamba ya panya."SUA tunataka kuipeleka teknolojia hiyo mpya katika mikoa inayolima mpunga kama vile Morogoro ,Iringa,Mvomero na Kilombero.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Jambo moja kubwa ni kuwa hatuna tabia ya kuwageuza hawa jamaa kuwa kitoweo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...