Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
MAMLAKA ya Mapato nchini (TRA) wamefanikiwa kukusanya jumla ya shilingi Trilioni 15.5 kwa mwaka mzima wa fedha 2017/2018 kuanzia julai 2017 hadi Juni 30 2018 ukilinganisha na shilingi trilioni 14.4 zilizokusanywa mwaka wa fedha 2016/2017.

Akizungumza na waandishi wa habari  leo Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi Richard Kayombo ameeleza kuwa kiasi kilichokusanywa ni sawa na asilimia 7.5 kiukuaji na kwa mwezi Juni pekee TRA imekusanya shilingi trilioni 1.5 ukilinganisha na trilioni 1.4 zilizokusanywa mwezi Juni mwaka 2017.

Aidha ameeleza kuwa sababu za kuongezeka kwa makusanyo hayo ni pamoja na uwepo wa elimu ya kodi inayowasaidia walipakodi na wananchi kwa ujumla kutambua umuhimu wa kulipa kodi, kuwa karibu na walipa kodi sambamba na kutatua changamoto zao za kikodi, kuongezeka kwa walipa kodi wapya  kupitia kampeni ya kuwasajili kwa kuwafuata waliko na kurahisisha ulipaji wa kodi kwa njia ya kielektroniki.

Pia ameeleza kuwa kwa mwaka huu wa fedha TRA imedhamiria kutekeleza kwa vitendo kampeni kabambe ya msamaha wa riba na adhabu kwa malimbikizo ya madeni ya nyuma na wanataraji kuongeza urahisi wa kulipa madeni ambayo yalikuwa kikwazo kwa wafanyabiashara wengi kulipa na hata kuendelea na biashara.

Kayombo amesema kuwa wamedhamiria kuongeza kasi ya usajili wa walipakodi wapya na wanaendelea na kasi ya utambuzi na usajili wa wafanyabiashara wadogo ili kila mtu anayestahili kulipa kodi asajiliwe na kuchangia kikamilifu maendeleo ya taifa.

Kwa niaba ya mamlaka hiyo amewashukuru na kuwapongeza walipa kodi wote ambao mchango wao umeiwezesha serikali kupata mapato ambayo yatasaidia shughuli mbalimbali za kimaendeleo kama vile ujenzi wa miundombinu,  upatikanaji wa elimu, afya na mambo mengine mengi yenye manufaa kwa watanzania wote.

Kayombo ametoa wito kwa walipa kodi wote kuendelea kulipa kodi kwa hiari na kujenga utamaduni wa kutoa na kudai risiti za kielektroniki na kutolea risiti (EFDs.)
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi Richard Kayombo akizungumza na waandishi wa habari wakati wa utoaji wa taarifa ya makusanyo ya kodi kwa mwaka wa fedha 2017/2018.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...