Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii
Mahakama ya Tanzania imesema haina sababu ya kugombana na Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) kwani mahakama haiwezi kuishi bila mawakili na wao hawawezi kuishi bila  mahakama. 
Msajili Mkuu wa Mahakama, Catherine Revocati ameyasema hayo wakati 
Uongozi wa TLS chini ya Rais wake, Fatuma Karume ulipokutana na Jaji Mkuu leo Julai 24.2018 kukubaliana  kushirikiana katika mabadiliko ya Tehama.

Msajili Revocati amesema,  mahakama ipo katika dira ya Mpango Mkakati wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), ambayo inahusisha wadau wote wa mahakama.

Amesema hatua hiyo inalenga kuondokana na mfumo wa kutumia makaratasi, ambapo mabadiliko hayo yanapaswa kuhusisha wadau wote wa kisheria ikiwemo TLS. 

Ameongeza kuwa, wameona ni vema wakashirikiana na TLS hasa katika upande wa Tehama, kwani hawana sababu ya kugombana maana Mahakama haiwezi kuishi bila Mawakili na hata wao mawakili hamuwezi kuishi bila mahakama,
Msajili Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Katarina Revocati akimkaribisha Rais wa TLS pamoja na Viongozi wengine TLS alioambatana nao alipotembelea Mahakama ya Rufani mapema Julai 24.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma akiongea jambo na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS),  Fatma Karume pindi Rais huyo pamoja na Viongozi wengine wa Chama hicho walipomtembelea Jaji Mkuu ofisini kwake Mahakama ya Rufani jijini Dar es Salaam mapema Julai 24, 2018.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma (wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), Fatma Karume (katikati) na viongozi wengine wa Chama hicho.
Rais wa TLS na Viongozi alioambatana nao wakifuatilia kwa makini mada kuhusu Mpango Mkakati na Maboresho ya Mahakama ilitolewa na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Maboresho-Mahakama, Bw. Sebastian Lacha.
Msajili Mkuu, Mahakama ya Tanzania,  Katarina Revocati akifafanua jambo, kushoto ni Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS),  Fatma Karume.
Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Fatma Karume akitoa neno la shukrani mara baada ya majadiliano katika ya TLS na Mahakama, katika majadiliano Viongozi hao wameahidi kufanya kazi kwa ushirikiano, katikati ni Msajili Mahakama ya Tanzania,  Katarina Revocati na kulia ni Mtendaji, Mahakama ya Rufani (T), Bw. Solanus Nyimbi.(Picha na Mahakama)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...