Na Tiganya Vincent, Tabora
HALMASHAURI ya Wilaya hapa nchini zimetakiwa kutenga maeneo kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo wadogo wa shughuli mbalimbali kwa ajili ya kuwasaidisa kukopesheka na asasi za kifedha.

Ombi limetolewa jana na Mwenyekiti wa Bodi ya  Mpango wa kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA).aliyemaliza muda wake Captain Mstaafu  John Chiligati wakati akiongea na uongozi wa Wilaya na ule  Halmashauri ya Wilaya ya Urambo.

Alisema uongozi wa Halmashauri umekuwa ukitumia fedha nyingi zake katika kuwalipa posho Mgambo ambao wamekuwa wakifukuza wafanyabiashara wadogo wadogo wakiwakuta wamepanga biashara katika maeneo ambayo sio rasmi badala ya kutumia fedha hizo kwa ajili ya kutenga eneo ambalo watawekwa pamoja ili kuendesha shughuli zao.

“Nawaomba Halmashauri tengeni maeneo ambayo mtawapanga wafanyabiashara kulingana na shughuli zao …kama ni mvua nguo mtaweka sehemu Fulani…kama anauza viatu atakuwa eneo lake ili kuwafanya watu wa Benki iwe kwao rahisi kuwakopesha…benki haziwezi kukopesha mtu anayetembeza bidhaa”alisema.
 Mkuu wa Wilaya ya Urambo Angelina Kwingwa akitoa salamu za Wilaya jana mara baada ya Wajumbe wa Bodi ya Mpango wa kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) wa sasa na baadhi ya waliomaliza muda wao kutembelea Wilaya hiyo kwa ajili ya makabidhiano na kutembelea wanufaika.
 Mratibu wa Mpango wa kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA)  Seraphia Mgembe akitoa ufafanua jana kwa wamefanikiwa urasimishaji wilayani Urambo  wakati Wajumbe wa Bodi ya Mpango wa kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) wa sasa na baadhi ya waliomaliza muda wao walipowatembelea.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Mpango wa kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) aliyemaliza muda wake Captian Mstaafu John Chiligati akitoa ufafanua jana kwa wamefanikiwa urasimishaji wilayani Urambo  wakati Wajumbe wa Bodi ya Mpango wa kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) wa sasa na baadhi ya waliomaliza muda wao walipowatembelea.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mpango wa kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) Balozi mstaafu Daniel ole Njoolay  akitoa ufafanua jana kwa wamefanikiwa urasimishaji wilayani Urambo  wakati Wajumbe wa Bodi ya Mpango wa kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) wa sasa na baadhi ya waliomaliza muda wao walipowatembelea. Picha na Tiganya Vincent.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...