Na Frankius Cleophace, Rorya

SERIKALI imemsimamisha kazi Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Kuruya katika Kata ya Komuge wilayani Rorya mkoani Mara Mwita Mangondi kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha Sh.1,960,387 ikiwa ni pamoja na kushindwa kusomea wananchi mapato na matumizi huku akipewa siku 19 kurejesha mara moja fedha hizo.

Ofisa Mtendaji huyo amesimamishwa kazi katika Mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Kuruya baada ya wananchi kutoa kilio chao cha muda mrefu kuhusu kutosomewa mapato na matumizi tangu Mwaka 2012 mpaka sasa.

Ambapo wamezidi kutupia lawama viongozi waliopo kuanzia ngazi za Vijiji hadi kata.Ofisa Utumishi Wilaya ya Rorya Peter Masanja akiwa katika mkutano huo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Charles Chacha amesema asimamisha kazi mtendaji huyo nakumpa siku 19 kurudisha fedha hizo. Pia anatakiwa kuripoti kila siku ofisi ya Mtendaji wa kata

Amesema kuwa kitendo cha Mtendaji huyo kufanya ubadhirifu wa fedha hizo kutokana na sheria za utumishi hawawezi kulifumbia macho hivyo amewataka wananchi kuwa wavumilivu kuhusu kumwondoa madarakani mwenyekiti wa Kijiji hicho kutokana na tuhuma walizozisema wananchi katika mkutano huo.

“Mimi Mamlaka niliyonayo ni ya kuondoa Mtendaji wa kijiji lakini sina mamlaka ya kuondoa Mwenyekiti nyie ndo wenye mamlaka mkifuata taratibu lakini kwa sasa mkimwondoa Halmashauri hautuafanya uchaguzi mpaka mwakani sasa baadhi ya maendeleo yatazidi kukwama niwasihi kuwa wavumilivu,” amesema.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Komuge William Nestory amesema kuwa endapo fedha hizo hazitarudishwa ataungana na wananchi kutoa taarifa eneo husika.Huku akiomba Ofisa utumishi kutilia mkazo kufanyika kwa mikutano ya kisheria ili wananchi wasomewe mapato na matumizi kwani suala hilo limekuwa changamoto kubwa katika vijiji vinavyounda kata yake.
Afisa utumishi Wilaya ya Rorya Mkoani Mara Peter Masanja akiongea na Wananchi katika Mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Kuruya kata ya Komuge Wilayani Rorya Mkoani Mara.
Wananchi wa kijiji cha Kuruya wakiwa katika Mkutano wa hadhara.
Wananchi wa kijiji cha Kuruya wakiwa katika Mkutano wa hadhara.
Mtendaji wa kijiji cha Kuruya Mwita Mangondi aliyesimamishwa Kazi katika Mkutano huo akijibu baadhi ya hoja za Wananchi zikiwemo tuhuma zake za ubadhilifu wa fedha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...