Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Michuano ya Sprite BBall Kings 2018 hatua ya robo fainali Imefikia patamu baada ya timu nane kufanikiwa kuingia na sasa kila mmoja kumfahamu mpinzani wake.

Katika droo hiyo iliyochezeshwa ikishuhudiwa na viongozi wa Shirikisho la Kikapu Nchini (TBF) iliweza kupangwa mbele ya viongozi na manahodha wa timu hizo.

Baada ya kumalizika kwa droo, michezo hiyo itachezwa tarehe  21 mwezi huu wa saba, kwenye Uwanja Wa Taifa Wa Ndani, Dar Es Salaam kuanzia saa 6 mchana hadi saa 2 usiku.

Timu zilizofanikiwa kuingia na kupangwa ni  Mchenga B Ball Stars dhidi ya  St. Joseph, Temeke Heroes dhidi ya Portland, Team Kiza dhidi ya DMI, pamoja na  Water Institute dhidi ya Flying Dribblers.

Michuano ya Sprite BBall Kings 2018 yanayodhamiwa na kinywaji cha Sprite yameanza mwanzoni mwa mwezi wa sita kwa hatua ya mchujo kufanyika, timu 16 kufanikiwa kuvuka na kupigwa mechi nane zilizokutana tena na  kisha kupatikana kwa timu nane zilizoingia robo fainali.

Mshindi wa kwanza atafanikiwa kuondoka na kitita cha Milioni 10 pamoja na Kombe, Mshindi wa pili milioni 3 na mchezaji bora wa mashindano  akitwaa milioni 2 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...