WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema baada ya mitatu Serikali itakuwa imefikia asilimia 90 ya lengo iliyojiwekea la kukuza uchumi kutoka wa chini hadi wa kati kwa kupitia sekta ya viwanda.

Amesema Serikali imedhamiria kukuza uchumi waTaifa na wa wananchi ili kufikia wa kati ifikapo 2025, hivyo amewaomba wananchi waendelee kuipa ushirikiano.Waziri Mkuu aliyasema hayo jana jioni (Alhamisi, Agosti 16, 2018) alipozungumza na wananchi katika kijiji cha Chomachankola wilayani Igunga akiwa katika ziara yake ya kikazi wilayani Igunga, Tabora.

“Tunaomba Watanzania waendelee kuwa watulivu na waipe ushirikiano Serikali yao katika kipindi hiki ambacho inaendelea kutekeleza ahadi yake ya kuinua uchumi,” alisema.Kadhalika, Waziri Mkuu alisema kuwa Serikali inaendelea na utekelezaji wa ahadi zote zilizotolewa na Rais Dkt. John Magufuli pamoja na zile zilizomo kwenye Ilani ya uchaguzi.

Waziri Mkuu alitaja ahadi hizo kuwa ni pamoja na ujenzi na ufufuaji wa viwanda vya kutengeneza bidhaa mbalimbali nchini, kikiwemo kiwanda cha kuchambua pamba cha Manonga.Alisema kiwanda cha kuchambua pamba cha Manonga ambacho kisimama kuchambua pamba kwa miaka 25 na sasa kimefufuliwa na kinafanya kazi, hivyo aliwaomba wananchi watoe ushirikiano kwa mwekezaji.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mitambo mipya ya kuchambua pamba inayofungwa katika kiwanda cha Manonga wilayani Igunga akiwa katika ziara ya kikazi mkoa wa Tabora Agosti 16, 2018. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa Tabora, Aggrey Mwanri. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama eneo inaposimikwa mitambo mipya ya kuchambua pamba katika kiwanda cha Manonga wilayani Igunga wakati alipokitembelea kiwanda hicho akiwa katika ziara ya kikazi mkoa wa  Tabora, Agosti 16, 2018. Kiwanda hicho ambacho kilisimamisha uzalishaji miaka 25 iliyopita kimefufuliwa na wamiliki wake , Chama Kikuu cha Ushirika cha mkoa wa Tabora, Igembensabo na Kampuni ya M/S Rajani Metals and Machinery kutokana na hamasa kubwa ya uchumi wa viwanda inayofanywa na serikali. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Chomachankola wilayani Igunga akiwa katika ziara ya kikazi mkoa wa Tabora, Agosti 16, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...