Na Jeshi la Polisi

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro ametoa onyo kali kwa majambazi na wahalifu wengine hususani wanaotumia silaha za moto kuacha mara moja kabla ya kukutana na moto mkali wa Jeshi la Polisi ambapo pia ametoa wito kwa wazazi kuwakanya watoto wao kujihusisha na vitendo hivyo.

IGP Sirro ameyasema hayo wakati akizungumza na Wakazi wa Mto wa Mbu Tarafa ya Manyara Wilayani Monduli Mkoani Arusha wakati wa Ziara yake mkoani humo yenye lengo la kubaini changamoto za kiuhalifu na kuzitafutia ufumbuzi.Alisema hivi sasa ujambazi wa kutumia silaha umepungua kwa kiasi kikubwa na baadhi ya matukio ambayo yamekuwa yakijitokeza yanaendelea kudhibitiwa na Jeshi la Polisi.

“Nawasihi wanaofikiria kuendelea kufanya vitendo vya uhalifu ikiwemo vya utumiaji wa silaha na kuua watu waache mara moja kwa kuwa wakikutana na moto wa Jeshi la Polisi wasije wakajilaumu mana kwa sasa moto wetu ni mkali hivyo nawashauri wazazi wakanye watoto wao” Alisema Sirro.

Aidha amewataka Wakazi wa Mto wa mbu Wilayani Monduli kuendelea na shughuli zao kama kawaida kwa kuwa usalama umeimarishwa katika kupambana na wahalifu waliokuwa wakifanya vitendo vya kuwaua watu hususani wanawake ambapo katika kipindi cha hivi karibuni kuliripotiwa matukio kadhaa ambayo yalileta wasiwasi katika eneo hilo muhimu kwa utalii.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akizungumza na na Wakazi wa Kata ya Mto wa Mbu Wilayani Monduli katika mkutano wa hadhara wakati wa Ziara yakeya kikazi Mkoani Arusha yenye lengo la kutatua changamoto za uhalifu (Picha na Jeshi la Polisi).
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akikagua gwaride baada ya kuwasili Shule ya Polisi Moshi zamani CCP kwa ziara ya kikazi kuangalia mwenendo wa mafunzo chuoni hapo na kuzungumza na Wakufunzi wa chuo hicho. (Picha na Jeshi la Polisi).
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akisalimiana na Maofisa waliopo Shule ya Polisi Moshi zamani CCP wakati wa ziara ya kikazi kuangalia mwenendo wa mafunzo chuoni hapo na kuzungumza na Wakufunzi wa chuo hicho. (Picha na Jeshi la Polisi).
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akisalimiana na Wakazi wa Kata ya Mto wa Mbu Wilayani Monduli wakati alipokwenda kuzungumza nao wakati wa Ziara yakeya kikazi Mkoa wa Arusha yenye lengo la kutatua changamoto za uhalifu (Picha na Jeshi la Polisi).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...