Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.

TAASISI ya Maendeleo ya jimbo la Vunjo(VDF) imesema gharama zilizotengwa awali kwa ajili ya ukarabati wa Km 272.8 za barabara katika vijiji vyote vya jimbo hilo huenda zikaongezeka kutokana na kuwepo kwa miamba katika maeneo ambayo yanahitaji upanuzi.

Katibu wa taasisi hiyo,James Mbatia amesema ikiwa imengia wiki ya tatu tangu kuanza kwa ukarabati kwa baadhi ya maeneo katika barabara hizo tayari wamekutana na changamoto ya uwepo wa miamba ambayo imelazimika kuvunjwa kwanza .

“Tulipanga hii kazi kutumia miezi sita kuimaliza lakini sasa inaweza kuchukua hadi mwaka mmoja kutokana na changamoto ambazo zimeanza kujitokeza hizi za kukutana na miamba na wakati mwingine hali ya hewa”alisema Mbatia.

Mbatia ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Vunjo alisema awali walipanga kutumia kiasi cha Sh Bil 7.29 kukamilisha kazi hizo lakini kwa namna shughuli inavyoendelea huenda gharama ikazidi huku akiendelea kutoa wito kwa wadau kuendelea kuchangia

“Hadi sasa tunashukuru kazi inaendelea vizuri tukishirikiana nawenzetu wa TARURA,TANESCO na tasisi nyingine ,lakini kipekee niombe serikali ione umuhimu wa kusaidia katika kutatua changamoto hii ya barabara kwa wakazi hawa wa jimbo la Vunjo”alisema Mbatia.

Kutokana na kuendelea kwa shughuli ya ukarabati wa barabara hizo tayari wananchi katika vijiji vya Shira na Mshiri vilivyopo katika jimbo la Vunjo wameanza kunufaika na mradi huo unaotekelezwa na Taasisi ya Maendeleo ya jimbo la Vunjo (VDF).Shughuli ya upanuzi wa barabara katika kijiji cha Mshiri,Marangu ikiendelea kwa uondoaji wa miti iliyo kando ya barabara ya awali sambamba na uondohaji wa Miundo mbinu ya umeme ili kupisha shughuli za upanuzi.

Michuzi Blog imefika katika maeneo mbalimbali ya vijiji vilivyoko katika jimbo la Vunjo na kujionea mitambo ikiendelea na shughuli za upanuzi wa barabara pamoja na uondoaji wa miti na mawe makubwa yaliyokuwa katika maeneo ya barabara hizo.
Katibu wa Taasisi ya Maendeleo ya Jimbo la Vunjo,James Mbatia akitoa salamu kwa baadhi ya wananchi walioshiriki katika ukarabati wa miundo mbinu ya barabara unaoendelea katika jimbo hilo kwa kuchangia nguvu kazi.
Mafundi kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wakiondosha Nyaya ili kupisha upanuzi wa barabara hizo.
Upanuzi wa barabara mbalimbali ukiendelea katika jimbo la Vunjo. 
Moja ya eneo ambalo kazi ya upasuaji wamiamba ililazimika kufanyika ili kupanua barabara .
Muonekano wa barabara katika maeneo mbalimbali wakati ukaraba huo ukiendelea .


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...