Na Emanuel Madafa ,Michuzi Blog -Mbeya 

Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya limeanzisha Msako wa kuwakamata watu wanaodaiwa kufanya uharibifu wa miundombinu ya maji huko katika Kijiji cha Ngole Kata ya Ilungu Wilaya ya Mbeya, Jeshi hilo tayari limeanza kutekeleza agizo hilo

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Urlich Matei amesema zoezi hilo ni utekelezaji wa agizo la Mkuu wa Mkoa wa Mbeya .

Amesema Agost 15 mwaka huu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila akiwa katika kikao cha baraza la madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, alitoa agizo kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwenda kukamata wananchi wanaodaiwa kuvamia na kuharibu mradi wa maji wa kijiji jirani.

Amesema kufuatia agizo hilo, Jeshi la Polisi limeanza msako katika cha kijiji cha Ngole kuhakikisha wale wote waliohusika na uharibifu huo wanakamatwa na kufikishwa Mahakamani kwa kosa la uhujumu uchumi.

Inadaiwa kuwa uharibifu uliofanywa na wananchi hao ni kukata mabomba yaliyokuwa yametandazwa kuanzia kwenye chanzo cha maji kwenda kwenye makazi ya Kijiji jirani wakitumia vifaa mbalimbali yakiwamo majembe na mapanga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...