*Ni baada ya upotevu wa sh. milioni 141 za kijiji

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Kamanda wa TAKUKURU wa wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Bw. Francis Zuakuu kumkamata aliyekuwa Mtendaji wa Kijiji cha Bulagamilwa, Bw. Ntemi James kwa tuhuma za kuhusika na upotevu wa sh. milioni 141 za kijiji hicho.

Ametoa agizo hilo leo (Alhamisi, Agosti 16, 2018) wakati akizungumza na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Igunga, akiwa katika siku ya kwanza ya ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani Tabora.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo baada ya Mbunge wa Manonga, Bw. Seif Gulamali kumuomba awasaidie katika kulipatia ufumbuzi suala hilo la upotevu wa fedha za kijiji kwa kuwa ni la muda mrefu na hakuna hatua zilizochukuliwa.

Kutokana na malalamiko hayo Waziri Mkuu amemtaka kamanda wa TAKUKURU wa wilaya hiyo ahakikishe anawatafuta watu wote waliohusika na upotevu wa fedha hizo za kijiji akiwemo na alitekuwa mtendaji wa kijiji cha Bulagamilwa, ambaye kwa sasa ni Mtendaji wa kata ya Igurubi.

Katika hatua nyingine,Waziri Mkuu amewataka watumishi wa umma wilayani Igunga wahakikishe wanatimiza wajibu wao ipasavyo kwa kuwatumikia wananchi kwa weledi na ustadi bila ya ubaguzi wa aina yoyote.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Igunga mkoani Tabora kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo, Agosti 16, 2018. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Igunga, John Mwaipopo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Baadhi ya watumishi wa Halmahauri ya wilaya ya Igunga wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao Kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo, Agosti 16, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi  wa Halmashauri ya wilaya ya Igunga mkoani Tabora kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo, Agosti 16, 2018. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Igunga, John Mwaipopo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...