*Awataka Marekani kuheshimu uhuru kamili wa Taifa letu
*Asema chaguzi hizo zimefanyika kwa misingi ya kisheria

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dk.Bashiru Ally ameamua kutoa msimamo wa Chama hicho kuhusu taarifa iiliyotolewa na Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania kuhusu uchaguzi mdogo wa Jimbo la Buyungu pamoja na kata 71 uliofanyika hivi karibuni.

Baada ya kufanyika kwa uchaguzi huo ambao CCM imepata ushindi mkubwa , Ubalozi wa Marekani waliamua kutoa taarifa kwa vyombo vya habari wakionesha kutoridhishwa na mwenendo wa uchaguzi huo.

Hivyo Dk.Bashiru Ally leo amezungumzia taarifa hiyo ya Ubalozi wa Marekani ambapo amesema ameisoma na kuilewa na wao kama Chama wanazingatia zaidi uhuru wa kitaifa na wanayo dhama ya kuulinda.

“Kauli ambayo wameitoa inagusa maeneo mengi na matarajio yangu taasisi zote zinazohusika zitazingatia madukuduku yao.

“Ninachojua mimi chaguzi hizi zimefanyika kwa misingi ya kisheria na mataifa mengine likiwamo la Marekani wanapaswa kuheshimu chaguzi zetu,”amesema Dk.Bashiru Ally.Mbali ya kauli hiyo ya Dk.Bashiru pia wachambuzi waliobobea kwenye medani za siasa nchini akiwamo Dk.Benson Banna wameonesha kusikitishwa na taarifa hiyo ya ubalozi wa Marekani nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...