Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

Aliyekuwa mhasibu wa Chuo cha ustawi wa Jamii, Gryson Mnyawami, amehukumiwa kwenda jela miaka mitano baada ya kupatikana na hata wizi wa zaidi ya sh. Milioni 9 akiwa mtumishi

Hukumu hiyo, imesomwa leo Agosti 15,2018 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na Hakimu Mkazi Mkuu Janeth Mtega,

Akisoma hukumu hiyo, hakimu Mtega amesema upande wa mashtaka kupitia mashahidi wake watano wameweza kuthibitisha pasipo kuacha shaka kuwa mtuhumiwa ametenda kosa la wizi.Hata hivyo, kabla ya kusomwa kwa hukumu hiyo, Hakimu Mtega alitaka mwendesha mashtaka kusema kumbukumbu kama mshtakiwa anamakosa mengine au  La

Mwendesha Mashtaka, wakili wa Serikali Janeth Magoho ameieleza mahakama kuwa, hakuna kumbukumbu za makosa kwa mshtakiwa, hili ni kosa lake la kwanza.Mheshimiwa Hakimu, sina kumbukumbu za zamani za mshtakiwa, ila naomba mahakama kutoa adhabu kali kwa kuwa kitendo cha wizi alichofanya mshtakiwa haswa akiwa kama mtumishi wa umma ni kibaya, kinaitia hasara kubwa Serikali

Wakili Janet ameongeza, suala la wizi katika Chuo cha ustawi limekuwa likitokea mara kwa mara Kitendo cha yeye kudhulumu wanafunzi siyo haki kwani ile ni hela ya walipa kodi, adhabu kali itakuwa fundisho kwake na kwa wengine wenye tabia kama hiyo

Katika utetezi wake, mshtakiwa Mnyawami, ameiomba mahakama hiyo kumpunguzia adhabu, alikubali kulipa fedha hizo taratibu lakini taasisi ndiyo ilimkatalia,Ameongeza kuwa Dada yake ni mgonjwa na mama yake ni mjane na wote wanamtegemea yeye.

Awali ilidaiwa, May 31, 2014 katika Chuo cha ustawi wa jamii kilichopo Kijitonyama wilayani Kinondoni mtuhumiwa akiwa ameajiriwa kama mhasibu wa Chuo hicho aliiba sh, 9,714,000 Mali ya muajiriwa wake ambayo  ameipata kutokana na nafasi yake kazini hapo,

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...