WAZIRI wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya makazi, William Lukuvi amezindua mpango wa kupimwa jumla ya vijiji 392 vinavyopakana na hifadhi za Taifa nchini kwenye mikoa mitano kwa lengo la kutatua migogoro ya ardhi katika maeneo hayo.

Waziri Lukuvi akizungumza katika uzinduzi huo, uliofanyika Babati mkoa wa Manyara alisema mpango huo utasaidia kutatua migogoro baina ya vijiji na hifadhi lakini pia vijiji kuwa na mpango wa matumizi bora ya ardhi.

Alisema, katika mpango huo, awamu ya kwanza itahusisha vijiji 95 katika mikoa mitatu nchini ila lengo ni kufikia mikoa mitano ya Manyara, Mara, Simiyu, Dodoma na Arusha.

“Vijiji hivi vikipimwa vitakuwa na mpango wa matumizi bora ya ardhi ambapo maeneo ya makazi yatajulikana maeneo ya mifugo na maeneo ya kilimo yatatengwa” alisema .Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Japhet Hasunga,alisema Wizara hiyo, imejipanga kushirikiana na Wizara ya ardhi na wadau wengine kutatua migogoro ya ardhi.

Alisema mpango wa kupima vijiji 392 vinavyopakana na TANAPA utakuwa ni shirikishi na utasaidia sana kutatua migogoro ya uhifadhi lakini utasaidia vijiji. “Katika mpango huo,zitatolewa hati 2375 ambazo zitasaidia wananchi kumiliki maeneo yao” alisema.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akizungumza mjini Babati jana kwenye kikao cha uzinduzi wa mpango wa matumizi bora ya ardhi ya vijiji vinavyopakana na hifadhi za Taifa, kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga. 
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akizungumza mjini Babati kwenye uzinduzi wa mpango wa matumizi bora ya ardhi ya vijiji vinavyopakana na hifadhi za Taifa uliofanywa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi. 
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti (kulia) akimuongoza Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi, William Lukuvi kwenye uzinduzi wa mpango wa matumizi bora ya ardhi ya vijiji vinavyopakana na hifadhi za Taifa jana mjini Babati. 
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti akizungumza mjini Babati kwenye uzinduzi wa mpango wa matumizi bora ya ardhi ya vijiji vinavyopakana na hifadhi za Taifa uliofanywa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...