Na Stella Kalinga, Simiyu

Zaidi ya wananchi 2000 wa Kijiji cha Lagangabilili wilayani Itilima Mkoani Simiyu wamenufaika na mradi wa maji safi na salama na kuondokana na adha ya kutumia muda mrefu kutafuta maji kwa kusogezewa huduma ya maji karibu na makazi yao.

Hayo yamesemwa na Mhandisi wa Maji wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu, Goodluck Masige wakati akitoa taarifa kwa kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2018, Ndg. Charles Francis Kabeho, aliyefika katika mradi wa maji wa Lagangabilili wenye thamani ya shilingi milioni 967, kwa ajili ya kufungua.

Masige amesema Mradi wa Maji wa Lagangabilili ulianza kutekelezwa mwaka 2015 na kukamilika mwaka 2018 na kuanza kutumika huku akibainisha uwezo wake kuwa, una kisima chenye uwezo wa kutoa maji lita 15,000/= kwa saa, vituo vya kuchotea maji 23 na mtandao wa maji wenye urefu wa mita 29,431.

“Kukamilika kwa mradi huu wakazi 2228 wanapata huduma ya maji safi na salama kwa ajili ya kunywa na matumizi mengineyo,mradi umepunguza muda waliokuwa wanaoutumia wananchi kutafuta maji kwa kuwasogezea huduma ya maji karibu na makazi kwa saa 24,mpaka sasa kaya 25 na taasisi za Umma 20 zimeunganishiwa maji” alisema Masige .

Awali Mkuu wa Wilaya ya Itilima Mhe. Benson Kilangi amesema kuwa tangu Uhuru eneo hilo lilikuwa halina maji kabisa, na baada ya kupatikana kwa huduma hiyo kutapunguza adha ya uhaba wa maji, huku akibainisha kuwa Serikali inategemea mradi mkubwa kutoka Ziwa Victoria kuwa suluhisho la kudumu la changamoto ya maji ka ajili ya matumizi ya binadamu na wanyama pia.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2018, Ndg. Charles Francis Kabeho akimtwisha ndoo ya maji Bi. Perusi Makeleja Mkazi wa Kijiji cha Lagangabilili wilayani Itilima mara baada ya kufungua mradi wa maji utakaowahudumia zaidi ya wananchi 2000, katika mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo leo Agosti 15, 2018.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2018, Ndg. Charles Francis Kabeho akifungua bomba la maji kujiridhisha ikiwa linatoa maji kabla ya kuzindua mradi wa maji wa Lagangabilili wilayani Itilima wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo, Agosti 15, 2018.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2018, Ndg. Charles Francis Kabeho akiweka Jiwe la Msingi Maboresho ya Kituo cha Afya Ikindilo wilayani Itilima mkoani Simiyu, wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo, Agosti 15, 2018. 
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2018, Ndg. Charles Francis Kabeho (wa pili kulia) akiangalia baadhi ya vifaa vya maabara ya Somo la Bailojia katika Shule ya Sekondari Budalabujiga kabla ya kufungua vyumba vitatu vya maabara vya shule hiyo wilayani Itilima, wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo, Agosti 15, 2018.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...