Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MEYA wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amepokea ugeni wa viongozi mbalimbali wa Jiji la Kampala nchini Uganda wakiongozwa na Waziri wa Jiji hilo Bennie Namugwanya Bugembe ambao wamekuja kujifunza na kupata uzoefu wa kuendesha na kusimamia shughuli za Jiji.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Meya Mwita amesema anaamini viongozi hao kuna mambo mengi watajifunza kwa kipindi ambacho watakuwa katika Jiji hilo huku akiwahakikisha watapata kila wanachokitaka.

Mwita amesena kuna mambo mengi mazuri ambayo yanefanyika na yanaendelea kufanyika katika Jiji la Dar es Salaam hivyo viongozi hao wa Jiji la Kampala kuna mambo watajifunza kwa ajili ya kuliboresha Jiji lao huku akiwahimiza kibuni vyanzo vipya vya mapato ili fedha zitakazopatikana wazitumie kufanya maendeleo.

Amesema kuwa ni vema wakatambua Jiji la Dar es Salaam kupitia viongozi wake wa ngazi mbalimbali wamefanikiwa kutatua changamoto mbalimbali ikiwamo ya usafiri kwa kuanzisha huduma ya usafiri wa mabasi ya mwendo kasi pamoja na treni ya Jiji.

"Nafahamu kuna mambo mengi ya kujifunza kutoka Jiji la Dar es Salaam,hivyo niwaombe mtakapokuwa hapa kila ambacho mnataka kufahamu basi kuweni huru kuuliza watalaam na viongozi wetu ambao wapo tayari kutoa majibu.

" Tumeweka mfumo mzuri katika kukusanya kodi ni vema mkajifunza na mtakaporudi Kampala muweke mikakati ambayo itasaidia kuwaongezea mapato na hatimaye mtafanya maendeleo kwa ajili ya wananchi ambao wamewachagua,"amesema Mwita.


Baadhi ya viongozi wa Jiji la Kampala nchini Uganda wakiwa kwenye ofisi za Meya wa Jiji la Dar es Salaam ambao wamekuja kujifunza namna ya kusimamia shughuli za Jiji

Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita(kulia) akiwa na Waziri wa Jiji la Kampala nchini Uganda Bennie Namugwanya Bugembe ambaye yupo katika Jiji hilo kwa lengo la kujifunza na kubadilisha uzoefu wa kusimamia shughuli za Jiji


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...