Na. Vero Ignatus. ARUSHA

Watanzania wameshauriwa kuenzi mila na desturi nzuri ili kuzirithisha kwa vizazi vijavyo na kuwa na Taifa lenye utamaduni madhubuti.

Rai hiyo imetolewa katika tamasha linalokutanisha familia 172 zenye jumla ya watu 323 kutoka katika kabila la wanyambo kutoka wilaya za Karagwe na Kerwa waishiao mkoani Arusha. Akizungumzia lengo la tamasha hilo mwenyekiti kikundi cha Kanono Wilbard Ngambeki amesema lengo kubwa ni kuimarisha umoja na kuzifanya familia zilizozaliwa kufahamu tamaduni zile nzuri za wazazi wao.

'' Katika tamasha hili michezo imekuwa ni kivutio kikubwa, wazazi wanawaleta watoto wao ila sisi tunapitisha mila zetu na desturi zetu njema kwao ili wakue wakitambua wazazi wao ndipo tulipotoka hata watakapokuwa kwenye miji mingine ya watu mbali na wazazi wao.''

Ngambeki amesema umoja huo wa Kundi la Kanono tayari walishaanzisha Saccos ambayo inawanachama 105 waliojiunga na tayari wameshakopeshana zaidi ya milioni 800 kwa riba nafuu. Afisa Ushirika Jiji la Arusha Huruma Kibendwa aliyekuwa mgeni rasmi katika tamashaa hilo amepongeza umoja kwa kuwa na saccos ambayo inawasaidia kukopeshana wao kwawao na kujikwamua kiuchumi na kimaendeleo

'' Kwani mara nyingi tunawashauri wanamchi wajiunge kwenye vikundi ili waweze kujikwamua kiuchumi kwa kukopeshana wao kwa wao mkopo wenye riba nafuu uzuri kikundi hiki kimesajiliwa na mna saccos inayofanya vizuri '' Alisema Kibendwa.
Mgeni rasmi Afisa Ushirika Jiji la Arusha Huruma Kibendwa akimkabidhi cheti mmoja wa kundi la Kanono, aliyepo kushotonkwake ni Mwenyekiti wa Kundi la Kanono Wilbald Ngambeki, na wakwanza kulia ni Davis Kalegea mtendaji wa kundi hilo. 
Wakina mama pamoja na wanaume kutoka kabila la Wanyambo waishio mkoani Arusha wakifanya maandalizi ya kutengeneza vyakula vya asili katika tamasha hilo. Picha na Vero Ignatus
Maandalizi ya chakula cha asili yakiendelea kama inavyoonekana pichani.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...