Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe, ameuagiza Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoa wa Njombe kumchunguza mkandarasi wa Kampuni ya China Henan International Cooperation (CHICO), anayejenga barabara ya Njombe-Moronga yenye urefu wa KM 53.9 kwa kiwango cha lami kama ana wataalaamu wa kutosha.

Waziri Mhandisi Kamwelwe ametoa agizo hilo katika wilaya ya Wanging’ombe mara baada ya kukagua hatua zilizofikiwa katika mradi huo na kutoridhishwa na kasi ya ujenzi wake ambapo mpaka sasa umefikiwa kwa asilimia 14.Mhandisi Kamwelwe amesema hana uhakika na kampuni hiyo kama ni wenyewe CHICO waliozoeleka katika uendeshaji wa miradi mingi hapa nchini hasa ya barabara.

“Sijaridhishwa na kasi ya huu ujenzi, Meneja wa TANROADS hakikisha unafuatilia kwa makini mradi huu na kubaini sababu zilizopelekea kusuasua kwa mradi na kuondoa wataalamu ambao wataonekana wanaudhaifu na kukwamisha mradi huo”, amesisitiza Mhandisi Kamwelwe.

Amebainisha kuwa hakuna sababu ya mkandarasi huyo kuchelewesha mradi huo kwani vifaa na mitambo yote ipo katika eneo la kazi na tayari Serikali imeshamlipa fedha alizozidai kwa asilimia 95.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, (wa pili kushoto) akizungumza na Mbunge wa Jimbo la Wanging’ombe, Gerson Lwenge (wa pili kulia), Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole-Sendeka (kushoto) wakati akikagua ujenzi wa barabara ya Njombe-Moronga yenye urefu wa KM 53.9, mkoani humo. Kulia ni Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Njombe Mhandisi Yusuph Mazana.
Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole-Sendeka akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa barabara ya Njombe-Moronga yenye urefu wa KM 53.9, mkoani humo.
Mhandisi kutoka kampuni ya Smec International Pty, Adarsh Nayyari, akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (katikati), ukubwa wa kazi unaoendelea wa kupasua mlima unaofanywa katika mradi wa ujenzi wa barabara ya Moronga-Makete KM 53.5 kwa kiwango cha lami, mkoani Njombe.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, akitoka kukagua moja ya kalvati katika mto wa Lyamadovela lililopo katika barabara ya Moronga-Makete yenye urefu wa KM 53.5 inayojengwa kwa kiwango cha lami, mkoani Njombe.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...